Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, Dr Mohamed Gharib Bilal alipowasili JNICC iliyopo sehemu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mahafali ya Kuhitimu Kidato cha Sita cha Mwaka 2022 ya Shule ya Feza kwa Wanafunzi wa Kike na Wakiume.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ambaye pia ni Mgeni Rasmi kwenye Mahafali ya Kuhitimu Kidato cha Sita cha Mwaka 2022 ya Shule ya Feza kwa Wanafunzi wa Kike na Wakiume akizungumza wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ambaye pia ni Mgeni Rasmi kwenye Mahafali ya Kuhitimu Kidato cha Sita cha Mwaka 2022 ya Shule ya Feza kwa Wanafunzi wa Kike na Wakiume akikabidhi cheti cha Taaluma kwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri kwenye Masomo Careen Nehemia Mwenisangale katika ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafuzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika Mahafali ya Wahitimu wa Kike na Wakiume wa Kidato cha Sita wa Mwaka 2022 wa Shule ya Feza kwenye ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam,
.......................................................
Na Mwandishi wetu,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiepusha na matendo maovu yanayokiuka Maadili ya Kitanzania yatakayowapelekea kuwa wateja wa Polisi na kukatisha ndoto zao.
Naibu Waziri Sagini ambaye ni Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kuhitimu Kidato cha Sita cha Mwaka 2022 ya Shule ya Feza amewakumbusha kutii Sheria bila shuruti na kuhakikisha wanafuata mienendo na nidhamu nzuri waliyofundishwa wakiwa shuleni.
“Mmeingia kwenye Ulimwengu ambao mkitenda maovu Sheria lazima ikuandame, huku hakuna ‘Suspension’ wala msamaha kutoka kwa wazazi” alisema.
Naibu Waziri Sagini alisema hayo Mei 28, 2022 wakati wa Mahafali hayo katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.
Aidha Naibu Waziri Sagini amewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kutumia vyema elimu yao waliyoipata katika kushiriki kwenye masula mbalimbali ya maendeleo ya jamii.
Akiwapongeza wazazi na walezi waliofika kwa kazi nzuri wanayoifanya Naibu Waziri Sagini amewakumbusha kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 itakayofanyika Agosti 23, na kusaidia Serikali kupata takwimu sahihi zitakazosaidia kupanga mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
0 Comments