Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF.SEDOYEKA AFUNGA MAADHIMISHO YA SABA YA WIKI YA UTAFITI NA UBUNIFU UDSM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Mei 26,2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-UTAFITI Prof.Bernadeta Kilian akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Mei 26,2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Bonaventure Rutinwa akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Mei 26,2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka akikabidhi tuzo kwa washiriki wa Wiki ya Utafiti ambao miradi yao imeshinda katika kuingiza fedha nyingi chuoni wakati wa kufunga Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Mei 26,2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Baadhi a wadau wa Tafiti na Ubunifu wakifuatilia hafla ya kufungwa kwa Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Mei 26,2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Vyuo Vikuu nchini vimetakiwa kujitokeza hadharani na kuonesha kazi zao za utafiti na ubunifu kwa umma hatua ambayo itavutia na kushawishi ufadhiri na ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kushiriki katika kuchangia rasrimali nyingi zaidi kwa ajili ya kuendeleza utafiti nchini.

Ameyaema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka wakati akifunga Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Mei 26,2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimepanua wigo wa Wiki hii ya Utafiti kwa kuwajumuisha washirika wa utafiti, ambao miradi yao imesajiliwa na ina mfungamano na idara mbalimbali za Chuo.

"Watafiti na wabunifu, tuna jukumu kubwa la kufanya utafiti na ubunifu unaolenga kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunatekeleza azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa kati imara na unaoendeshwa na sekta ya viwanda". Amesema Prof.Sedoyeka

Aidha Prof.Sedoyeka amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kujenga imara uchumi unaotegemea viwanda ambavyo sio tu vitatumika kuzalisha bidhaa na huduma za kutosheleza mahitaji ya Watanzania, bali viwanda hivyo vitatumika kuongeza ajira kwa kizazi cha sasa na kijacho na pia kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nje ya nchi na hivyo kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-UTAFITI Prof.Bernadeta Kilian amesema Maonesho hayo yalihusisha wanataaluma na wanafunzi kushiriki kuonesha shughuli na miradi yao mbalimbali ya utafiti na ubunifu katika ngazi husika.

Amesema Prof.Kilian amesema katika ngazi hiyo, kulikuwa na jumla ya washiriki 869 kati yao idadi ya wafanyakazi ilikuwa ni 419 (48%) na wanafunzi ilikuwa ni 450 (52%).

"Jumla ya kazi za utafiti na ubunifu zilizooneshwa na kuwasilishwa ni 269. Mhe Mgeni Rasmi, hili ni ongezeko la miradi 51 ukilinganisha na mwaka 2021 ambapo kulikuwa na miradi 218". Amesema

Post a Comment

0 Comments