Meneja wa NHIF Ally Mwakababu akiofafanua huduma zinazotolewa na mfuko huo nchini zinavyowqfikia watu wa makundi yote katika ngazi zote.
***************
Na Hamida Kamchalla, Tanga.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) imeongeza huduma zake katika kuhakikisha kila Mtanzania kutoka makundi mbalimbali kuweza kutumia Mfuko wa Bima ya Afya kwenye matibabu katika ngazi zote.
Akizungumza kwenye maonesho ya biashara na utalii yanayoendelea mkoani Tanga, Meneja wa NHIF Ally Mwakababu amesema bima ya afya ndio pekee inayoweza kuwapa wananchi uhakika wa matibabu.
"Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya ndio Taasisi pekee inayoweza kutoa uhakika huduma ya Afya juu ya uhakika wa matibabu, hili ni eneo ambalo unaweza kukutana na wananchi wa aina mbalimbali juu ya matibabu" alisema Mwakababu
"Mwanzoni tulikua tunatoa huduma kwa ajili ya watumishi wa serikali kuu, ikaja watumishi wa serikali za mitaa, ikaja mashirika, vyomba vya usalama lakini bado serikali ikawa inahitaji wananchi ndani ya Mfuko wa Bima ya Taifa kama unavyojua huduma za Afya ni ghali" aliongeza.
Mwakababu amebainisha kwamba kwa sasa wamengeza huduma zaidi ambapo kunamakundi ya watoto, wakulima walioko kwenye vyama vya msingi (amcos) pamoja na wafanyabiashara, lakini pia NHIF inatoa huduma mbalimbali za kupima Afya kama Sukari, presha, uzito wa kupindukia na huduma zote ni bure.
"NHIF imekua na vifurushi ambavyo mwananchi atachagua mwenyewe, ninajali, wekeza na timiza ambapo mteja anachagua mwenyewe kutokana na namna anavyotaka kuhudumiwa" amesema.
0 Comments