Ticker

6/recent/ticker-posts

MSD IFUMULIWE YOTE NA SI MENEJIMENTI PEKE YAKE’- CHIKOTA



****************************

MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota ametaka Bohari ya Dawa(MSD) ifumuliwe ipasavyo na isitazamwe menejimenti peke yake.

Kauli hiyo ameitoa bungeni jijini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka 2022/23.

Chikota amesema wafanyakazi wa kati wana uwezo wa kumkwamisha Mkurugenzi wa taasisi hivyo ni bora ikafumuliwa.

“MSD wanasambaza dawa ukiona kama kuna madereva wanaotaka kukwamisha utendaji kazi anauwezo wa kumwambia Afisa utumishi huyu ni CEO wa nane kwenye hii taasisi na akashindwa kupeleka dawa kwa wakati, kufumuliwa kwa MSD kusiwe ni kwa bodi na menejimenti pekee, twende hadi madereva na watumishi wa kati,”amesisitiza

Kuhusu upotevu wa dawa, Chikota ametaka udhibitiwe hasa kwa wanaojificha kwenye mgongo wa madawa.

“Bajeti ya MSD inapaswa kuongezwa na tulifanya marekebisho ya sheria kwamba wanaweza kujenga viwanda vya dawa, wa mradi pale Keko ambao unahitaji mtaji ili wazalishe dawa zenye ubora na kuuza nchi jirani,”amesema.

Pia Mhe.Chikota , amempongeza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa kutoa takwimu za kweli kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa ambayo kwasasa ni asilimia 51.

“Nakupongeza Waziri maana huko nyuma tulikuwa tukiletewa takwimu lakini kuhalisia hazikuwa za kweli umeona badala ya kuwadanganya watanzania umeamua kusema ukweli,”amesema.

Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maagizo aliyoyatoa kuhusu MSD na kwamba kuna kazi ya kufanyika kwa kuwa mafanikio ya taasisi hayategemei menejimenti.

Post a Comment

0 Comments