Ticker

6/recent/ticker-posts

MKE WA MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Mbonimpaye Mpango akiongoza mbio maalum “Run For Hedhi Salama” zilizoandaliwa na Jukwaa la Hedhi Salama maalum kwa kukuza uelewa kwa jamii juu hedhi salama na kuchangia upatikanaji wa huduma salama za hedhi. Mbio hizo zimefanyika katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama duniani leo tarehe 28 Mei 2022.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Mbonimpaye Mpango (Mwenye kiremba cha rangi ya bluu) akisikiliza maelezo kutoka kwa wawezeshaji wa maabara ya Hedhi salama mkoani Kigoma wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama Duniani leo tarehe 28 Mei 2022.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Mbonimpaye Mpango akivalishwa skafu maalum ya shujaa wa Hedhi Salama wakati wa Maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama Duniani yaliofanyika kitaifa mkoani Kigoma leo tarehe 28 Mei 2022.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Mbonimpaye Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Hedhi Slama Tanzania wakati wa Maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani yaliofanyika kitaifa mkoani Kigoma leo tarehe 28 Mei 2022.

Post a Comment

0 Comments