Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AKIWA ZIARANI SWEDEN


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 31 Mei 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Arlanda, Stockholm nchini Sweden ambapo anatarajia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Juni 2022 nchini humo. Pembeni ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mheshimiwa Grace Olotu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 31 Mei 2022 akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mheshimiwa Andres Sjoberg wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Arlanda,Stockholm nchini Sweden ambapo anatarajia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Juni 2022 nchini humo.

***********************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 31 Mei 2022 amewasili Stockholm nchini Sweden ambapo anatarajia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Juni 2022 nchini humo.

Dhumuni la mkutano huo ni kuchochea utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Ajenda 2030) hususani katika upande wa mazingira na kujadili namna ya kurejesha uchumi endelevu katika kukabiliana na janga la Uviko 19. Aidha mkutano huo ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika mkutano wa kwanza wa mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Stockholm mwaka 1972.

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali pamoja na wadau wa Mazingira Duniani.

Post a Comment

0 Comments