Ticker

6/recent/ticker-posts

KANUNI ZA UNUNUZI WA UMMA ZAZINDULIWA


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba, Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, wakati wa uzinduzi wa kanuni hizo, jijini Dodoma, kulia ni Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara hiyo, Dkt. Frederick Mwakibinga.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliokabidhiwa Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kulia), akimkabidhi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Lawrence Mafuru, Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kulia), akimkabidhi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Omolo, Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Eliakim Maswi, Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na wazabuni wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, baada ya kuzinduliwa, jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo na kamati ya uzinduzi wa Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Wizara hiyo baada ya uzinduzi wa Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

*****************************

Na. Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imezindua Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma ili kuhakikisha shughuli za ununuzi zinafanyika kwa kuzingatia uadilifu, uwazi, usawa na ushindani wenye tija katika ununuzi wa umma.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), aliwaagiza watumishi na wazabuni wanaoshiriki katika shughuli za ununuzi wa umma kuzingatia Kanuni hizo kwakuwa Serikali haitosita kumchukulia hatua yeyote atakayefanya kinyume.

“Leo katika uzinduzi huu tunaweka meno ya kuwangáta wale wote watakao kwenda kinyume na Kanuni kwa mujibu wa Sheria, meno haya hayatangáta si tuu watumishi wa umma, bali yatangáta wale wote watakao husika”, alisisitiza Mhe. Chande.

Alisema ununuzi wa Umma ni eneo muhimu katika matumizi ya fedha za Serikali kwa sababu linabeba zaidi ya asilimia 50 ya bajeti ya Serikali kila mwaka huku akitolea mfano wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22 ambapo bajeti ya ununuzi ni shilingi trilioni 20.48 sawa na asilimia 56 ya bajeti yote ya Serikali.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel M. Tutuba alisema Serikali imetunga Kanuni hizo ili kudhibiti changamoto mbalimbali katika shughuli za ununuzi na ugavi nchini zinazosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo baadhi ya watumishi na hata wazabuni wanaoshiriki katika shughuli za ununuzi na ugavi kukosa maadili.

Alisema hayo yamethibitishwa na taarifa mbalimbali za kaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma zinazotolewa kila mwaka ambazo zimekuwa zikibainisha kuwepo kwa viashiria vya vitendo vya rushwa na kutozingatiwa kwa Sheria na Kanuni katika kutekeleza ununuzi na hivyo kuisababishia Serikali kupata hasara.

“Hata hivyo, hatua za kisheria zimeendelea kuchukuliwa kwa wote wanaobainika kushindwa kuzingatia Sheria katika kutekeleza ununuzi wa umma”, alibainisha Bw. Tutuba.

Alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango itaendaelea kusimamia na kuimarisha eneo la ununuzi na ugavi sambamba na kuongeza juhudi katika kupambana na vitendo vyote vinavyokinzana na maadili ya taaluma ya ununuzi na ugavi katika kutekeleza ununuzi wa umma.

Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga, alisema kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kuzindua kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma na Wazabuni Wanaoshiriki katika shughuli za Ununuzi wa Umma lengo la kuzindua Kanuni hizo ni kuhakikisha kunakuwa na usimamizi imara wa ununuzi wa umma na pia Kanuni hizo zimezingatia matakwa ya Sheria ya Ununuzi wa Umma SURA 410

Alisema kuwa Kanuni hizo zimeweka bayana misingi ya maadili wanayotakiwa kuyazingatia kila wanapotekeleza shughuli za ununuzi kwa kubainisha mambo ambayo wazabuni wanapaswa kuyatekeleza na yale ambayo hawapaswi kutekelezwa kila wanaposhiriki manunuzi yanayofanywa na Serikali ikiwemo kughushi nyaraka, kutoa siri za Zabauni na kupitisha zabuni bila kuzingatia taratibu.

Kwa kutunga Kanuni hizi, zinapanua wigo wa kuwabana washiriki wote wa zabuni wakiwemo watumishi wa Serikali na wale wa Sekta binafsi kwa kuwa awali kulikuwa na uwezekano wa vishawishi kutoka kwa wale ambao hawakubanwa na kanuni hizo.

Post a Comment

0 Comments