Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu mwenyekiti wa Sekta Binafsi (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Bi.Mercy Silla akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC),Godwill Wanga akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewezesha kutafuta fedha za kugharamia utekelezaji wa miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ambapo Wizara imetoa kiasi cha Bilioni 50 kwa halmashauri 55 ili kufanikisha mradi huu.
Ameyasema hayo leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula katika Mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi.
Amesema utekelezaji huo unafanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI.
Aidha amesema Wizara imewezesha upatikanaji wa mkopo wa benki ya dunia kiasi cha shilingi Bilioni 340.5 ambao pamoja na kazi zingine uttawezesha kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na Usalama wa miliki.
Hata hivyo amesema Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za utatuzi wa changamoto zinazojitokza ikiwemo, kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za ardhi, kuendelea kuimarisha na kuziwezesha Ofisi za Ardhi zilizopo katika kila mkoa katika kuhakikisha huduma zinapatikana karibu na wananchi.
"Wadau na wamiliki wote wa ardhi mtumie utaratibu wa ukadiliaji na upimaji kodi ya pango la ardhi ki-elekroniki kwa kuwa utaratibu huu ni rafiki, unaokoa muda na ni nafuu". Amesema Waziri Mabula.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi amesema kupitia mkutano huo watapokea maoni ya sekta binafsi kuhusu maboresha yanayotakiwa kufanyika kwenye sekta ya ardhi na lengo ikiwa ni kuchochea mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi jumuishi na kukuza maendeleo ya jamii na kuhakikisha uendelevu wa mifumo ya kimazingira.
"Sekta binafsi inamchango mkuwa kwenye maboresho ya sekta ya ardhi nchini kwani inatoa mchango mkubwa kwenye ubunifu, upatikanaji wa mitaji na uwekezaji ambao huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye shughuli za uzalishaji hasa katika sekta ya viwanda, kilimo, mifugo na shughuli nyingine nyingi za maendeleo". Amesema
Amesema ufanisi wa sekta hizi unategemea kwa kiasi kikubwa kuwa na mifumo ya usimamizi na uendelezaji wa sekta ya ardhi ambayo inaweza kujenga mazingira wezeshi bila kukwamisha mipango ya sekta nyingine.
Nae Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC),Godwill Wanga amesema wameanzisha mkutano huo ili kukutanisha Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali na wadau wa sekta binafsi ili kujadili changamoto, fursa na maboresho kwaajili ya kukuza mchango wa sekta katika maendeleo ya uchumi na jamiii nchini.
0 Comments