Ticker

6/recent/ticker-posts

DIPLOMASIA YA UCHUMI YA RAIS SAMIA KUIBUA KIWANDA CHA MBOLEA NCHINI


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo akizungumza jambo wakati wa hafla ya jaribio la mbolea itakayozalishwa na kiwanda cha Intracom kinachojengwa Jijini Dodoma kikiwa na uwezo wa kuanza kuzalisha tani laki sita za mbolea kwa mwaka.Mkurugenzi wa kiwanda cha Intracom Fertilizer Limited, Nduwimana Nazaire akizungumza jambo wakati wa hafla ya Majaribio ya mbolea itakayozalishwa na kiwanda chake kinachotarajiwa kuanza uzalishaji mwezi Julai 2022 na kuzalisha kiasi cha tani laki sita za mbolea kwa mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Taanzania (TFRA) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majid Hemed Mwanga (haonekani pichani) walipokuwa wakikagua mashamba kujionea tofauti ya uzalishaji katika mashamba yaliyopandwa na kukuziwa kwa mbolea aina ya DAP na UREA na mbolea inayozalishwa na kiwanda cha Intracom kinachozalisha mbolea yenye mchanganyiko wa samadi na kemikali(organic fertilizer) tarehe 19/5/2022.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania Dkt. Godfrey Mkamilo(wa kwanza kulia) akieleza matokeo ya jaribio la mbolea aina ya fomi pandia na fomi kuzia baada ya kuitumia katia mashamba darasa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majid Hemed Mwanga(wa kwanza kushoto) tarehe 19/5/2022 alipotembea ili kujionea matokeo ya mbolea itakayozalishwa na kiwanda cha mbolea cha IntracomViongozi mbalimbali walioshiriki hafla ya jaribio la mbolea itakayozalishwa na kiwanda cHa Intracom wakifuatilia hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za kijiji cha Ilonga tarehe 19 Mei, 2022 wilayani Kilosa.

**************

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Majid Hemed Mwanga amekiri kuwa diplomasia ya uchumi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan imekuwa sababu ya kumpata mwekezaji wa kiwanda kikubwa cha mbolea cha Intracom Fertilizer Limited kinachojengwa Jijini Dodoma.

Alisema, Rais Samia ni Rais mwenye maono asiyependa kuzungumza na badala yake amejikita katika matendo zaidi.

Mkuu wa Wilaya Mwanga aliyasema hayo jana tarehe 19 Mei, 2022 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kueelimisha wakulima wa eneo la Ilonga wilayani Kilosa Mkoani Morogoro juu ya namna mbolea inayozalishwa na kiwanda hicho inavyofanya kazi katika kuongeza tija kwenye kilimo.

Kupitia mashamba darasa yaliyopandwa kwa tutumia mbolea itakayokuwa ikizalishwa na kiwanda hicho inayojulikana kama fomi pandia, fomi kuzia pamoja na mbolea iliyozoeleka ya DAP na Urea zimetumika katika mashamba darasa yaliyopo katika scheme ya umwagiliaji wa zao la mpunga ililopo katika kijiji cha Ilonga Kata ya Chanzulu wilayani Kilosa ili kuonesha utendaji wa mbolea hizo na kuwafanya wakulima wachague mbolea sahihi kwao.

Kufuatia kuwa, mbolea itakayozalishwa kiwandani hapo itakuwa na mchanganyiko wa samadi na kemikali kwa uwiano sawa kutafungua fursa kwa wafugaji kukusanya samadi inayotokana na kinyesi cha ng'ombe na kukiuzia kiwanda hicho.

"Samadi sasa hivi ni mali tutapata tenda ya kukusanya samadi na kupeleka kiwandani itazalisha mbolea na mkulima atatumia mbolea na kupata mavuno mengi yatakouzwa nje ya nchi na kutuingizia pesa za kigeni" Mwanga alikazia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Dkt. Geofrey Mkamilo alisema taifa lina matumaini makubwa na mbolea itakayozalishwa na Itracom Fertilizer Limited katika kutatua changamoto ya upatikanaji na bei ya mbolea nchini.

Hata hivyo alisema TARI inaendelea na utafiti wa kuona utendaji wa mbolea hiyo ambapo wanaangalia ulinganifu wa kiasi kinachowekwa kwenye mazao na matokeo yake na baadaye kuwaeleza wananchi matokeo ya utafiti huo.

Alisema, pamoja na kujaribu mbolea hiyo katika eneo hilo pia wamefanya katika maeneo mengine nchini. "Tumeanza kufanyia majaribio ya mbolea hapa Ilonga kwa zao la mpunga, zao la alizeti na mtama homboro, zao la maharage na mahindi eneo la Siriani mkoani Arusha na mkoani Mbeya kwa zao la mahindi, maharage, viazi na mpunga", Dkt. Mkamilo alisisitiza.

Aliendelea kusema, Taasisi anayoisimamia inaendelea na zoezi la kupima afya ya udongo nchi nzima na tayari mikoa 18 imeshapimwa wanaendelea kukamilisha kwa mikoa 8 iliyosalia ili kufahamu udongo una rutuba ya kiasi gani na umepungikiwa na kitu gani kulingana na mahitaji ya zao husika na si kuweka mbolea kwa kubuni tu ili kuwa na kilimo chenye tija.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo alisema kujengwa kwa kiwanda kikubwa cha mbolea nchini kutatatua changamoto ya upatikanaji na bei ya mbolea kwa wakulima.

Aliongeza kuwa utashi wa kisiasa nchini upo vizuri na kutoa wito kwa wawekezaji wengine katika eneo la mbolea kuja kuwekeza nchini.

"Malighafi kwa ajili ya kulisha viwanda vya mbolea zipo, nishati ipo, nguvu kazi ipo na soko lipo hivyo wafike kuwekeza" Dkt Ngailo alikazia.

Pamoja na hayo aliwataka waingizaji, wazalishaji na wauzaji wa mbolea nchini kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku ili waweze kushiriki kwenye kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa kiwanda cha Intracom Fertilizer Limited, Nduwimana Nazaire aliwahakikishia wakulima wa Ilonga na Tanzania kwa ujumla upatikanaji wa mbolea na kubainisha kuwa bei ya mbolea itakayozalishwa kiwandani hapo itakuwa nzuri ukilinganisha na aina nyingine za mbolea zinazoingizwa nchini kutoka maeneo mbalimbali duniani.

"Msiwe na shida na mashaka mbolea itapatikana na itakapotosheleza mahitaji ya ndani ndipo tutaisafirisha kwenda nje ya nchi" Nazaire anasema.

Kwa upande wake mkulima aliyetoa shamba lake litumike kwa mafunzo hayo aliishukuru TARI kwa kupeleka mradi huo katika kijiji chao na kukiri mbolea ni kilio cha wakulima wa eneo la kilosa.

Alisema, wakulima wa Kilosa wamefurahia sana ujio wa kiwanda hiki nchini kwani wanaamini watakuwa wanufaika wa kwanza kwa kupata bidhaa hiyo adhimu ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji katika shughuli zao za kilimo.

Post a Comment

0 Comments