************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Coastal Union ikefanikiwa kutinga hatua ya Fainali kombe la Azam Sprots Federation Cup mara baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya timu ya Azam Fc.
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa dakika 90 kwa timu zote bila kupata bao na kufanya kwenda dakika 30 za nyongeza nako timu hazikupata bao nakwenda hatua ya mikwaju ya penati.
Katika mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha uliibua hisia kubwa za mashabiki kwani timu zote mbili zilionesha kandanda safi japokuwa walitengeneza nafasi nyingi za wazi bila mafanikio.
Sasa Coastal Union wanatinga hatua ya fainali ambapo watakutana na Yanga Sc mchezo ambao utapigwa katika dimba hili la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
0 Comments