Ticker

6/recent/ticker-posts

CAG: WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI KUFICHUAA UBADHILIFU WA FEDHA ZA UMMA

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles Kichere akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari wakati akitoa taarifa ufunguzi wa mkutano wa kwaida wa kuwajengea uwezo ili waweze kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya CAG.
Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile akizungumza kwenye mkutano huo.
Mhariri Jackton Manyerere akizungumza kwenye mkutano huo.
'
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira Emmanuel Mubuguni akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Wahariri wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.








Na Dotto Mwaibale







MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles Kichere ameviomba vyombo vya habari kuandika habari za uchunguzi ili kusaidia Serikali kubaini mianya ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kachere ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwaida wa kuwajengea uwezo ili waweze kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya CAG.

"Waandishi wa habari ni wadau wakubwa sana katika kuhabarisha jamii kuhusu shughuli mbalimbali tunazozifanya hasa katika eneo la utawala bora hivyo tunahitaji ushirikiano wenu" alisema Kachere.

Alisema waandishi wa habari wanakazi kubwa ya kimkakati wanayo ifanya katika jamii kama ilivyo mihimili mingine katika kuhabarisha umma habari mbalimbali kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.

Akijibu maswali kuhusu sheria ya manununuzi alisema imekuwa na changamoto kubwa na mapungufu kadhaa ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali.

Alisema sheria hiyo inatakwa kufanyiwa mabadiliko ili kuisaidia Serikali na akasema wsimamizi wa sheria hizo wanatakiwa kuwa waadilifu ili kazi isonge mbele.

Akielezea kuhusu suala la mazingira alisema kuna kila sababu ya kuongeza nguvu katika eneo hilo na akakiomba chama cha waandishi wa habari za mazingira (JET) kuhamasisha jamii kuhusu uhifadhi wa mazingira na kuwa ofisi ya CAG itaongeza kasi ya ukaguzi vinginevyo nchi itageuka kuwa jangwa.

Alijibu suala la vitisho alisema ofisi yake haiogopi vitisho vya mtu yeyote kwani wanafanya kazi kwa uhuru na kwa mujibu wa sheria na wapo kwa jili ya kufanya kazi za Serikali na kuangalia maslahi ya Taifa na wananchi na kuwa wamekuwa na ushirikiano mzuri dhidi yao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasa katika eneo la manunuzi.

Post a Comment

0 Comments