**************************
Chama cha waongoza watalii Zanzibar ZATO wameandaa tamasha la Utamadani la Afrika (FESTAC AFRICA) ambalo linalenga kukusanya na kuziunganisha Nchi 54 za Afrika ili kuonyesha sanaa na utamaduni ambao unapatikana katika bara la Afrika
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa ZATO Hassan Ally Mzee amesema lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha Waafrika na kujumuika pamoja ili kuweza kutangaza utamaduni wa Afrika kwa Mataifa mengine.
Pia Mzee amesema Mataifa mengi ya Afrika yatashiriki katika tamasha hilo kutakuwa na muziki wa bendi pia makongamano yatakayokuwa na wasemahi wakuu mbalimbali wakiwemo Marais wastaafu Jakaya Kikwete,Abeid Aman Karume, Mohammed Ally Shein,Rais mstaafu wa Botswana ,mabarozi na watu maarufu.
Sanjari na hayo Mzee amewataka Waafrika kuhakikisha wanadumisha utamaduni na kulinda maeneo ya kihistoria kwa kutangaza kwenye vyombo vya habari.
Kwa upande wake mwenyekiti wa maonyesho hayo Yinka Abioye,amesema walifikilia namna ya kuwaunganisha waaafrika wote pamoja wakaona waje na tamasha la kitamaduni kwasababu kila mwafrika anatamaduni zake hivyo ni lazima watawaunganisha kwa pamoja na lengo kuu la tamasha hili ni kuunganisha Bara la Afrika.
Katika matukio yatayoambatana na tamasha kutakuwa na Mkutano wa biashara lengo lake ni kukuza uelewa na mbinu za kibiashara za washiriki na kila mtu anakaribishwa kushiriki katika matukio yote.
Aidha katika Tamasha hilo kutaambatana na matukio mbalimbali ikiwemo maonyesho ya biashara makongamano yatayoongozwa na watu mashuhuri wakiwemo maraisi wastaafu ikiwa ni pamoja na michezo mbalimbali.
0 Comments