*********************
Na Emmanuel Kawau.
Jamii hususani vijana wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti ili kudhibiti uharibufu wa mazingira na kuboresha hali ya hewa Dunia.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Joan itanisa Meneja mawasiliano wa shirika la uhifadhi mazingira WWF katika maadhimisho ya siku ya sayari ya Dunia ambapo amesema WWF wameshirikiana na chuo cha ustawi wa jamiii katika maadhimisho hayo kwa kupanda miti mia moja.
Joan ameongeza kuwa ujumbe wa mwaka huu katika maadhimisho haya ni wekeza katika sayari yetu ya dunia, WWF imekuwa ikishirikisha vijana katika zoezi la upandaji miti na kuhifadhi mazingira na mpaka sasa wameshapanda miti zaidi ya Elfu kumi.
"Na huu ni mwendelezo wetu wa kuunga mkono kampeni iliyoanzishwa na ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira chini ya Waziri seleman jafo ya soma na mti ambapo inaelekeza kila mwanafunzi kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu anapanda walau mti mmoja lakini sisi tunasema haishii tu kupanda basi anapokuwa shuleni qma chuo anahakikisha anautunza mti ule mpaka unakua" alisema Joan
Kwa upande wake Mwakilishi wa mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Andrew Randa amesema miti ni sehemu muhimu katika utunzaji wa mazingira Dunia ya leo imekumbwa na ongezeko la joto na yote hiyo inatokana na uhalibifu mazingira hususani ukataji wa miti pasipo kupanda mwingine.
Aidha amesema kusudi kubwa la maadhimisho hayo ni kuhamasisha watanzania wengi zaidi kujitokeza katika zoezi la upandaji miti kila siku katika maisha yao ili kuhakikisha mazingira yanalindwa ipasavyo.
Nae mmoja wa wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii mickdad uhuru amewaomba wanafunzi wenzake kuunga mkono kampeni ya upandaji miti na kufanya swala hilo kuwa sehemu ya majukumu yao.
0 Comments