Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdlah Ulega mara baada ya kutua na helikopta mkoani Tanga wakati timu ya Mwaziri wa Wizara za Kisekta ilipokwenda kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi ya vijiji 975 katika mkoa huo tarehe 2 April 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiongoza ujumbe wa Mawaziri wenzake wa Wizara za Kisekta baada ya kutua na helikopta mkoani Tanga walipokwenda kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwenye mkoa huo tarehe 2 April 2022.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akizungumza kwenye kikao na uongozi wa mkoa wa Tanga wakati timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula ilipokwenda mkoani humo kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwenye mkoa huo tarehe 2 April 2022. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.
Sehemu ya washiriki wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Tanga kuhusu utatuzi utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kilichofanyika mkoani Tanga tarehe 2 April 2022.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi akichangia hoja wakati wa kikoa baina ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Tanga kuhusu utatuzi utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 2 April 2022.
Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow akichangia hoja wakati wa kikoa baina ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Tanga kuhusu utatuzi utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 2 April 2022 (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
**********************
Na Munir Shemweta na Magreth Lyimo, WANMM TANGA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makakzi Dkt Angeline Mbuala ametaka elimu na ushirikishwaji wananchi kupewa kipaumbele wakati wa utekeleza maamuzi ya Baraza la Mawiziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975
Dkt Mabula alisema hayo mkoani Tanga tarehe 02 April 20202 wakati yeye na timu yake ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakitoa mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa viongozi wa mkoa na wilaya katika mkoa huo kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi.
Katika maamuzi yake, Baraza la Mawaziri lilipendekeza vijiji 14 katika mkoa wa Tanga kubaki maeneo ya hifadhi na kufanyiwa marejebisho ya mipaka huku vijiji viwili na mitaa miwili kufanyiwa tathmni kutokana na sehemu kubwa ya maeneo yake kuwa na umuhimu kwa maslahi ya Taifa.
Katika mkoa wa Tanga maeneo yenye mgogoro wa matumizi ya ardhi yanahusisha wananchi na Hifadhi ya Msitu wa Mikoko na Shamba la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo katika Kituo cha TALIRI,
Maeneo mengine ni kwenye Hifadhi za Misitu Chang’andu, Kwani na Gendagenda pamoja na mgogoro katika Pori Tengefu la Mto Umba na ule wa Shamba la Mwele-ASA.
‘’Rai yangu katika utekelezaji maamuzi haya ya Baraza la Mawaziri ni ushirikishwaji ili asitokee mtu akalalamika kaonewa au kafanyaje, jukumu letu kama serikali ni kuhakikisha tunatoa elimu pia ili masuala haya yasijirudie kwa sababu tumekuwa na operesheni mbalimbali ambazo mwisho wa siku utekelezaji au usimamizi wake ubakuwa siyo mzuri sana’’
‘’Kipindi hiki Mhe mama Samia asingependa kuona masuala haya ya migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali yanajirudia ndiyo maana katika Wizara ya Ardhi ametoa fedha nyingi ili kumalizana na migogoro ya ardhi’’.
Hata hivyo, Waziri wa Ardhi alisisitiza suala la uwajibikaji kwa watendaji wa serikali kuanzia mkoa hadi kijiji na kuwataka kila mmoja kusimamia majukumu yake ili masuala ya uvamizi kwenye hifadhi na taasisi za umma yasijirudie.
‘’Tunaporekebisha maeneo haya hatutarajii tena uvunjifu wa sheria uendelee uongozi kuanzia ngazi ya kijiji muwe walinzi wazuri wa maeneo hayo ili kuepuka migogoro hiyo ya wananchi kujimegea maeneo ambayo siyo rasmi kwa makazi’’ alisema Dkt Mabula.
Mawaziri walioko kwenye ziara hiyo mkoani Tanga walielezea hatua na mikakati ya kuchukua wakati wa utekelezaji Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa Migogoro katika vijiji 975.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega alisisitiza suala la watendaji wa serikali kuwa imara wakati wa kusimamia zoezi zima la utekelezaji maamuzi hayo ili kuepuka kupata tabu kwenye utekelezaji.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Hamis Chillo aliwahimiza watendaji wa serikali kuhakikisha wanasimamia na kutunza mazingira hususan kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na kusisitiza utumiaji busara wakati wa utekelezaji maamuzi ya baraza la Mawaziri.
Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo alielezea mikakati ya serikali kupitia wizara yake katika kujikita kwenye uzalishaji mbegu ili kukidhi mahitaji ya nchi na kuepuka uagizaji mbegu kutoka nje ya nchi sambamba na kufanya utafiti katika mashamba yake yaliyovamiwa.
Waziri wa Ardhi Dkt Mabula ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Kisekta aliwaasa wananchi hasa waliotengewa maeneo yaliyowekewa mipango ya matumizi ya ardhi kuwa, serikali haitarajii kuona tena wakiingia maeneo ya hifadhi na vyanzo vya maji yaliyozuiliwa kwa kuwa uvamizi uliofanywa ndiyo uliosababisha migogoro ya matumizi ya ardhi.
‘Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Wizara yake isingependa kuona mambo haya yanajirudia na wale wote ambao mara nyingi wanavamia maeneo na kutarajia serikali kuridhia kuendelea wawepo maeneo hayo, suala hili halitajirudia tena na kinachotakiwa sasa kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa kutii sheria bila shuruti kwani serikali haiwezi kuwa na mazoezi haya kila mwaka.
0 Comments