Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZALISHAJI WA MATOFALI NCHINI WASHAURIWA KUFUATA MATAKWA YA VIWANGO

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Mhandisi Johaness Maganga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya TBS na wazalishaji na wasafirishaji wa matofali nje ya nchi katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS, Mhandisi Johaness Maganga akifungua mkutano kati ya TBS na wazalishaji na wasafirishaji wa matofali nje ya nchi katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam Baadhi ya Maafisa Viwango TBS, wakizungumza kwenye mkutano na baadhi ya wazalishaji na wasafirishaji wa matofali leo katika ukumbi wa TBS Jijini Dar es Salaam

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la viwango nchini Tanzania (TBS) limewakumbusha wazalishaji wa matofali na wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi kuwa TBS ndiyo wenye jukumu la kuweka na kusimamia viwango vya kitaifa hivyo kuhakikisha wanafuata utaratibu na sheria.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya TBS na wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Johaness Maganga amesema kuwa wao wana jukumu la kutoa mafunzo na ushauri viwandani juu ya uzalishaji wa bidhaa bora.

Aidha amesema kuwa jukumu lingine pia ni kupima na kuhakiki vipimo vinavyotumika viwandani pamoja na kuelimisha umma juu ya masuala yote yanayohusu uwekezaji na usimamizi wa viwango pamoja na udhibiti wa ubora wa bidhaa.

Katika hatua nyingine Mhandisi Maganga amesema kuwa TBS itaendelea kuandaa mikutano mbalimbali kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango.

Pamoja na hayo wadau walishukuru kwa jinsi ambavyo TBS imetambua umuhimu wakuwa na mkutano huo kwani wameongeza uelewa na waliahidi kufikisha kwa wenzao walioshindwa kufika kutokana na kutingwa na majukumu.

Post a Comment

0 Comments