Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Bi.Hilda Nkabe akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala ya waatoto wenye usonji nchini.
Daktari watoto wenye usonji Edward Kiria akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala ya waatoto wenye usonji nchini.
*********************
Na Magrethy Katengu-Dar es salaam
Imeelezwa kuwa licha ya jitihada zinazofanywa kuwasaidia watoto wenye usonji lakini bado watoto hao wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kunyanyapaliwa na jamii inayowazunguka ikiwemo familia ndugu kuonekana kama na ni laana na wengine hufungiwa ndani wasionekane kabisa
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayojuhusisha na watoto wenye usonji (Lukiza Autism Foundation) Hilda Nkabe amesema ifikapo tarehe 10/4/2022 mbio za usonji ili kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huo na kukusanya michango ya wadau mbalimbali ili kuwasaidia wazazi na familia zenye watoto wenye usonji.
"Tunataka kuwashawishi wazazi kuwa huru na watoto wao wenye matatizo ya usonji na wenye ulemavu mbalimbali na kuacha kuona kuo watoto ulemavu kuwa ni Jambo la laana"
Kwa upande Daktari anayeshughulika na watu wenye usonji Edward Kiria amesema katika miaka ya hivi karibu ugonjwa wa usonji umeonekana kuongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa Kati ya watoto miamoja Duniani mtoto mmoja anaugonjwa wa usonji.
Aidha amesema usonji unaathiri wa watoto katika hatua za ukuaji,kushindwa kuongea, kuchelewa kupata ufahamu,kushindwa kuwasiliana kupitia ishara,pia amesema zipo dalili za magonjwa mengine hususani ya mtindio wa ubongo ambapo dalili zake hufanana na usonji.
"Kuwahudumia watoto wenye ni gharama kwani wengine wakihudumiwa angalau viungo vyao viwe sawa kupitia huduma kutoka madaktari bingwa (specialistis ) mbio hizi tunawaomba wadau mtuchangie tuwasaidie kwani lengo tunaanza na watoto kumi"alisema Daktari Edward
Aidha katika mbio hizo kutakuwa usajili inayoendelea kufanyika Mlimani City kwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu thelathini na tano ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Aksoni na ni mbio za km5,10 na km 21 ambapo washindi katika mbio zote watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha na medani watu wote wanakaribishwa kushiriki katika hali na mali kusaidia
0 Comments