*************************
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kikao cha wadau wa ngozi hapa nchini.
Kikao hicho pia kiliwajumuisha pia wataalam kutoka Taasisi ya Ushirikiano ya Kijerumani GiZ leather technical team
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika tarehe 26 Aprili, 2022 lengo likiwa ni ajili ya kujadili hatua za awali za utekelezaji wa Mradi wa Support towards Industrialization and Productive Sectors ambapo Sekta ya ngozi ni miongoni mwa sekta za kipaumbele. Mradi huo utatekelezwa katika nchi wanachama wa SADC kwa ufadhili na Umoja wa Ulaya (EU).
TanTrade iliwakilishwa na wataalam Kadhaa wa Sekta ya ngozi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Bw.Emmanuel Miselya ambaye aliwaeleza wadau wa Ngozi nchini kuwa TanTrade ipo tayari kushirikiana nao kuhakikisha Sekta Hiyo inakuwa na kuleta tija Kwa wadau wote kuanzia mfugaji hadi muuzaji wa Bidhaa ya ngozi.
Kwa upande wake mtaalam kutoka GiZ Bw.Klaus Heinze amesema Sekta ya ngozi bado ina fursa kubwa kwa soko la ndani ya nchi Tanzania na katika soko la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kwani Bado bidhaa nyingi za ngozi zinaingizwa katika soko hilo kutoka mataifa ya mbali . Bwana Klaus aliongeza kuwa namna bora ya kuhakikisha Sekta hiyo inakuwa ni kuhakikisha mnyororo wa thamani (value chain) inasimamiwa ipasavyo kwa kila hatua .
Naye katibu Mtendaji wa Jumuiya ya wazalishaji wa Bidhaa ya ngozi nchini Bwana Freddy Kabala alitaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo kwenye Sekta Hiyo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ngozi zenye ubora ,Utaalam duni wa uzalishaji pamoja Mitaji. Bw.Kabala alieleza kuwa changamoto hizo zinapelekea bidhaa zinazozalishwa nchini kuonekana kuwa ghali na hivyo kupunguza uzalishaji na kisha kutoa mwanya kwa bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi ili kuziba pengo kubwa lililopo.
Tanzania inakadiriwa kuwa na ng'ombe zaidi ya 33.4 milioni na mifugo mingine kama Mbuzi na kondoo zaidi ya milioni 30 huku Uzalishaji wa viatu vya ngozi ni wastani wa jozi milioni tatu huku jozi milioni 54.3 za viatu vya ngozi vinaingizwa nchini kutoka mataifa mengine ya Ulaya na Asia kwa mwaka.
Mpaka Sasa kuna Viwanda vinne vikubwa vinavyozalisha bidhaa za ngozi nchini Tanzania , Viwanda hivyo ni Bora Industries, Woiso Original Products (WOP), Ital Shoes na Kilimanjaro Leather International Company Industries L.t.d
0 Comments