Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA IUCN KUWEZESHA VIKUNDI VINNE MKOPO WA SH. M 126, KUKUZA UCHUMI WA BLUU.

Baadhi ya wanachama wa vikundi vya wajasiriamali eakiea kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa hundi yao.


***************************

Na Hamida Kamchalla, Tanga.


Jumla ya sh. milioni 126 zinatarajiwa kuwawezesha wajasiriamali wa maeneo ya baharini katika kukuza uchumi wa bluu kupitia mradi wa kukuza ujasiamali na kuboresha maisha ya jamii zinazoishi maeneo ya Pwani lakini pia kulinda na kutunza ikolojia ya bahari.


Fedha hizo zilizotolewa na Ubalozi wa Ireland kupitia International Union for Conservation of Nature (IUCN) zinatajiwa kuviwezesha vikundi vinne ambavyo viwili ni vya wajasiriamali wa Wilaya ya Pangani kwa upande wa Tanzania Bara na viwili kutoka Wilaya ya mkoani Pemba.


Akizindua mradi huo, mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema matarajio ya Mkoa katika mradi huo ni kuona wananchi wanaoishi maeneo husika wananufaika na kubadili maisha yao kiuchumi.


"Wananchi mnaoishi katika maeneo hayo ndiyo mtakuwa kielelezo cha uchumi wa bluu baada ya mabadiliko yenu kimaisha, matarajio yaliyopo ni kuboresha maisha ya wananchi waishio katika maeneo hayo ya bahari ya Pangani na Pemba" alisema.


"Kwa Mkoa wa Tanga maeneo ya Pangani na Mkinga wanazalisha sana zao la mwani lakini sijui nini kinawakwaza, tutawaewezesha fedha hizi za mikopo lakini zikatumike kwa lengo lililokusudiwa la biashara na siyo kwa ajili ya kuolea, kuongeza mke" alisisitiza.


Malima alisema mradi huo ili ufanikiwe, mara baada ya mafunzo wanayopatiwa wajasiriamali hao ioneshe mafanikio ya kuendelea na wawe mfano darasa ili watu wengine waje kujifunza kutoka kwao, huku akitoa shukurani kwa IUCN kwa kuandaa programu yenye manufaa kwa wananchi lakini pia katika suala zima la utunzaji wa mazingira.


Kwa upande wake Meneja Miradi Mazingira na Tabianchi Ubalozi ea Ireland Fazal Issa alisema Ubalozi huo unasaidia Shirika la IUCN katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa uchumi wa bluu ambao umezinduliwa juzi unalenga kukuza wajasiriamali wadogo katika masuala ya uchumi.


"Lengo hasa, ukiliushanisha na kipengele cha Ireland ni kusaidia jamii kuweza kuboresha kuingizankipato chao, lakini pia kutunza rasilimali katika bahati na maeneo yanayoizunguuka Pwani" alisema Issa.


"Tumeangalia tafiti katika kipengele hiki cha kuwagusa wananchi wa maeneo hayo tukaona ni muhimu zaidi tukiamini kwamba maisha yao yanapokuwa Bora, itakuwa ni rahisi pia kusimamia rasilimali hisi, tumeona sababu ambazo zinachangia uharibifu wa rasilimali na maeneo ya bahari na fukwe ni watu kujitafutia kipato, ambapo wanakata miti ya mikoko, wanafanya uvuvi ambao siyo endelevu pamoja na kuharibu matumbawe" alibainisha.


Naye Meneja Mradi Coastal and Ocean Resielience (IUNC) Elinasi Monga alisema mradi huo ni wa majaribio wa meaka wa kwanza na unalenga kusaidia uendelezaji wa sera ya uchumi wa bluu kwa namna ambavyo utaleta ushiriki wa watu mbalimbali na katika kuhifadhi maeneo ya bahari na viumbe vya baharini kwa muda mrefu.


"Sasa ili kufikia lengo hili, mradi unatumia mikakati mikubwa minne, kuboresha mifumo ya kiutawala ya Taasisi ambazo zinahusiana na masuala ya uhifadhi wa bahari, zitatusaidia namna ambavyo tunasimamia bandari na mifugo ya bahari, lakini pia namna ya kuboresha maisha ya wananchi" alisema Monga.


Pia alibainisha kwamba, "kwasasa tumeanza kutoa sh milioni 126 kwa vikundi hivi vinne ambavyo vitapata mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kufanya shuhuli za kibiashara ya utengenezaji wa mpango wa biashara, usimamizi wa fedha, uwekaji wa kumbukumbu pamoja na uwezaji wa kufikia masoko na baadae watapata fedha kwa ajili ya kujiendeshea miradi yao".


Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini, Ofisa kutoka Wizara hiyo Ally Hamisi Shafi alisema uchumi wa bluu, uhimili wa mabadiliko ya tabianchi pamoja na uwezeshwaji wa Wanawake ni maeneo ya kipaumbele katika sera ya maendeleo ya Kimataifa ya Ireland.


"Vipaumbele hivi vimejumuishwa katika mpango mkakati mpya wa miaka mitano wa Ubalozi huu, sambamba na kipaumbele hiki, tutaimarisha kazi zetu katika uhimili wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uchumi wa bluu, masuala ya usawa wa kijinsia na uhimili wa mabadiliko ya tabianchi yana uhusiano mkubwa" alisema.


"Kwa sababu hizi, Ireland inajenga na kuimarisha ushirikiano katika miradi yake na washirika wake wanayotekeleza, kwa mfano hapa Tanga, Shirika la IUCN linatengeneza ushirikiano na Mashirika yanayotekeleza miradi inayosaidiwa na nchi hiyo ikiwemo chini ya UZIKWASA na TALIRI" aliongeza.

Post a Comment

0 Comments