Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KATIKA MWAKA 2021/2022 IMEFANIKIWA KUKAMATA MADINI YENYE THAMANI MILIONI 501.23 YALIYOKUWA YAKITOROSHWA

Msemaji wa sekta wizara ya madini kutoka Chama Cha ACT Wazalendo Edga Mkosamali akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam


*************************

Na Magrethy Katengu

Chama Cha ACT Wazalendo kimesema Serikali kupitia Wizara ya madini imekua ikihakikisha inaongeza jitihada za kupunguza wimbi la utoroshaji wa madini ambapo imefanikiwa kukamata madini yenye thamani ya shilingi milioni 501.23 katika mwaka 2021/2022 ambapo Wafanyabiashara wasiowaaminifu waliokuwa wakitorosha kuelekea nje ya nchi kupelekea kulikosesha Taifa mapato.

Akizungumza na Waandishi wa habari Msemaji wa sekta ya madini chama Cha ACT Wazalendo Edga Mkosamali mara baada ya Waziri wa madini Mhe Dotto Biteko kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo mwaka 2022/2023 bungeni Dodoma

ambapo amesema sekta ya madini licha upotevu wa Mapato yatokanayo na utoroshwaji wa madini lakini ni sekta iliyopanda kuchangia pato la Taifa kutoka asilimia 3.4 hadi kufikia 7.7 hivyo serikali haina budi kuziba myanya ya utoroshwaji wa madini ili ifikia asilimia 10

"Upotevu wa Mapato ya madini hutokana na serikali kutotekeleza matakwa ya sheria ya madini sura 123(marekebisho ya mwaka 2019) kipengele kinachoitaka katik kila shughuli ya uchimbaji wa madini leseni ya uchimbaji wa madini leseni Maalumu serikali iwe na hisa isiyopungua 16% katika mtaji wa kila kampuni ya uchimbaji madini"alisema Mkosamali

Hata hivyo ameitaka serikali kuanza kutenga fedha katika bajeti yake walau asilimia tano kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo Tanzania ambao huchangia asilimia 30 ya pato la taifa kupitia sekta ya madini ila hadi sasa serikali bado haiwajali ili hali sera inasema serikali itawezesha ili kukua kwa kuwaelimisha na kuwapatia mtaji na vifaa hivyo ni vyema serikali ikaanzisha benki ya madini ili isimamie mikopo na wachimbaji wadogo wa madini kwani ni vigumu kwa benki za kawaida kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo”

Aidha serikali imeshauriwa kushirikiana na sekta binafsi kupata suluhisho ya changamoto ya Nishati katika migodi kuachana na matumizi ya dizeli ili kusaidia Uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi

Post a Comment

0 Comments