Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya wadau wa Bandari ya Tanga walipotembelea bandarini baada ya kumalizika kwa kikao chao na mamlaka hiyo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud akizungumza wakati wa wadau wa Bandari ya Tanga kilichofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu Nikodemas Mushi
Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu Nikodemas Mushi akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara na kikao cha wadau wa Bandari ya Tanga
AFISA
Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC )Mkoani Tanga
Captain Christopher Shalua akizungumza jambo wakati wa kikao cha wadau
wa Bandari
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
BANDARI
ya Tanga inatarajiwa kuanza kupokea Meli za Magari ifikapo Mwezi Mei
mwaka huu ambayo yatakuwa yakipelekwa kuhifadhiwa eneo la Mwambani
Jijini Tanga .
Hatua hiyo inatajwa kwamba itafungua fursa mpya
za kiuchumi kwenye Bandari ambayo kwa sasa inafanyiwa maboresho makubwa
ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake.
Hayo
yalisemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud wakati wa
ziara ya wadau wa Bandari ya Tanga walipotembelea bandarini baada ya
kumalizika kwa kikao chao na mamlaka hiyo.
Meneja Mrisha alisema
eneo la mwambani lina ukubwa wa hekta 176 sasa kama walivyosema
wanatarajia kuhudumia shehena kubwa kutoka 750,000 mpaka kufikia Milioni
3000,000 hivyo mzigo utakuwa ni mwingi.
Alisema kutokana na
hilo wamependelea eneo hilo watalitumia kufanya shughuli za nyengine
ikiwemo kupakilia mizigo kwenye makontena na kuweka kontena tupu na
shughuli zinazoambatana na shughuli za kibandari
Hata hivyo
aliwaeleza wadau hao kuhusu maboresho ya Bandari ya Tanga ikiwemo jinsi
mradi wa maboresho ulivyo mpaka sasa awamu zote tatu ambapo awamu ya
kwanza ilikuwa ni kuongeza kina kutoka mita tatu mpaka mita 13 kwenye
mlango bahari,sehemu ya kujeuzia meli na vifaa ambapo iligharimu Bilioni
172.3.
Alisema pia wameona maboresho ya base mbili zenye urefu
mita 450 zilizogharimu Bilioni 256.8 na wameona ahadi iliyolewa na
mkandarasi ambapo mpaka mwezi Mei watakabidhiwa kipande cha mita 150 na
itakapofika octoba wakabidhi mita zote 450.
Hata hivyo alisema
kwamba hoja ambazo zimewasilishwa na wadau kwenye kkao hivho
wamezichukua na kwenda kuzifanyia kazi na wao wametusikiliza kuwaeleza
namna maboresho makubwa yaliyofanyika na kuhaidi kuitumia kwa ajili ya
kupitisha shehena zao.
Awali akzingumza mara baada ya ziara ya
wadau hao kwenye Bandari hiyo kushuhudia maboresho makubwa yaliyofanyika
Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania Makao Makuu Nikodemas Mushi alisema mkutano huo ulikuwa na nia
ya kukutana na wadau wanaohudumiwa na Bandari ya Tanga ambayo
inayohudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo nchi Jirani Rwanda.
Alisema
kupitia mkutano huo wanaamini watafungua ukurasa mpaya wa kiboshara na
lengo lao ni kuondoa nafasi ya maswali na hoja na changamoto mbalimbali
ambazo hazijaweza kutoka upande mmoja kwenda mwengine.
Kaimu
Mkurugenzi huyo wa Masoko na Uhusiano alisema wadau wametoa maoni huku
akieleza kwamba Meneja wa Tanga na timu yake wamesikia na wamejipanga
tayari kuanza kuzifanyia kazimara moja,.
Alisema na suala ambalo
linawahusu makao makuu watalibeba na kulipeleka huku ili yaweze
kufanyiwa maamuzi na huo ni mkakati wa kimasoko
Mwisho.
0 Comments