Ticker

6/recent/ticker-posts

MADEREVA PIKIPIKI NA BAJAJI WATAKIWA KUTII SHERIA BILA SHURUTI



**********************

Na Magrethy Katengu-Dar es salaam

Kikosi cha usalama barabarani kimewataka madereva wa pikipiki na bajaji kutii sheria bila shuruti ikiwemo kuvaa kofia ngumu(elementi), kuacha kubeba mishikaki ikiwa ni pamoja na kukatisha bararabarani wakati taa nyekundu inawaka.

Agizo hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na  Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Dar es salaam SACP Wilbrod Mutafungwa wakati wa kikao kilichowakutanisha Shirikisho la madereva waendesha pikipiki na bajaji Bodaboda ni kazi kama kazi nyingine hivyo ni lazima ifanyike kwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani.

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema watumiaji wengi wa barabara hususani bodaboda na bajaji hawazingatii sheria ya usalama barabarani kutokana na kujifunzia udereva mtaani hivyo jeshi la polisi limeamua kukutana nao kufahamu ni changamoto gani inayowapelekea kuvunja sheria hiyo na kuwa sugu na kusababisha kufanya kazi katika mazingira hatarishi

"Kwa kweli inasikitisha sana ukitembelea hospitali ya Taifa Mhimbili ukiwaona baadhi ya wagonjwa wakipata majeraha wengine wakiwa wamekatwa viungo vya mwili hawezi kabisa na nikilinganisha na wengine wakifanya mizaha na vyombo hivyo vya moto barabarani nawasihi kabla ya kutumia vyombo hivyo muende mkawaone wenzenu wanavyoteseka Moi .

Naye Muwakilishi wa Madereva wa bodaboda Amos Paulo kutoka Magomeni kanisani amesema kiukweli kazi hii kwa sasa imeingiliwa na baadhi ya madereva ambao siyo waaminifu wanafanya kazi hiyo pasipokuwa na elimu yeyote ya usalama barabarani na kupelekea kazi hiyo kutoheshimika hivyo tunaliomba Jeshi la polisi kukagua leseni za madereva ambao hawajaenda shule ili kusaidia kudhibiti tatizo la madereva holela kwa jina maarufu (Vishandu)

"Kazi ya madereva pikipiki baadhi ya watu ambao siyo waaminifu wameitumia kufanya vitendo vya kihalifu ikiwemo kubora simu,pochi na kubeba abiria kisha kwenda kuwapora mali zao "alisema Amosi

Naye Ally Amlani dereva bodaboda anayetokea Mbezi ambaye kazi anafanyia kituo cha Posta amekiri kuwa anabeba abiria mishikaki kutokana na hali ngumu ya maisha kutokana abiria wenyewe nauli wanayotoa hivyo inamlazimu kuwabeba mshkaki ili arudishe mafuta anayotumia kuja mjini.

Kwa upande wake Paul Kristian amesema kuwa kuna changamoto kubwa kwa makamada hao hasa pale urafiki askari anayekaa pale kuongoza magari amekua akiweka magari mda mrefu kukaa foleni na kuanza kukamata bodaboda zikiwa kwenye foleni hivyo kusababisha bodaboda kukatisha kwenye barabara wakati taa nyekundu zinawaka.

Aidha Wanaotumia vyombo vya moto wametakiwa kutii Sheria bila shuruti ili kusaidia kuepusha ajali zinazotokea bila sababu.

Post a Comment

0 Comments