******************
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amempongezq Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa kuwaletea wananchi maendeleo katika kupindi cha mwaka mmoja tu alichokaa madarakani.
Amesema kwa sasa Rais yuko katika nchini Marekani ambapo amesema ziara hiyo imemkutanisha na viongozi wakubwa akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ambaye nchi yake Ina ushawishi mkubwa duniani.
Kinana ameyasema mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa wana CCM wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.
"Sasa hivi anafanya ziara nje huko, kwa wafadhili, watoa mikopo, ili tuweze kupata fedha nyingi zaidi kwa maendeleo ya taifa letu.
"Rais yuko Marekani, ameonana na Makamu wa Rais wa Marekani. Marekani ni nchi kubwa, Marekani Ina kauli duniani, Marekani ni mshiriki wetu wa maendeleo katika sekta mbalimbali zinazowagusa wananchi," amesema.
Amesema Rais Samia pia amekutana na viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha duniani (IMF), Taasisi ambazo ni washirika muhimu wa maendeleo na uchumi wa Tanzania, hivyo anastahili pongezi.
0 Comments