Ticker

6/recent/ticker-posts

KEVELA AWATAKA WATANZANIA KUUNGA JUHUDI ZA SERIKALI HASA KUJITOKEZA KWENYE ZOEZI LA SENSA


********************

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi ili kuunga mkono juhudi zinazofaanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuiletea nchi maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akitoa salamu zake za Sikukuu ya Pasaka kwa wanawake wa Mkoa wa Njombe na watanzania kwa ujumla ambapo alisisitiza kuwa ni muhimu kwa kila mtanzania kushiriki kikamilifu katika mchakato huo ili kusaidia ukuaji wa maendeleo ya nchi kama ambavyo Rais Samia amesisitiza.

Mbali na kuwataka wanawake hao kusheherekea kwa amani na upendo sikukuu hiyo ya Pasaka, alisema zoezi la sensa lina manufaa makubwa kwa Taifa hivyo ni vyema wakajitokeza na kushiriki kikamilifu.

" Sensa ni muhimu, hauwezi kupanga maendeleo ya nchi kama hujajua idadi ya watu ulionao, Rais amesisitiza kuwa sote ni vyema tukajitokeza na kushiriki katika zoezi hilo Agosti 23 Mwaka huu, niwasihi tusimwangushe, tujitokeza kikamilifu"tv alisema Mama Kevela

Alisema kama Taifa kuna manufaa mengi ya kushiriki sensa hiyo, hivyo ni vyema kila mtu akaona umuhimu wake na kujitokeza siku hiyo kufanikisha suala hilo litakalotusaidia watanzania katika kujiletea maendeleo.

Aidha amepongeza ziara ya Rais Samia nchini Marekani sambamba na hotuba aliyoitoa mbele ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo Kamala Harris kwa kuwa inazidi kuhimarisha uhusiano baina yaa nchi hizo mbili.

Awali akizindua nembo ya sensa hiyo sambamba na tarehe ya kufanyika kwake, Rais Samia Suluhu Hassan alisesema zoezi hilo i muhimu kwa kuwa litaisaidia Serikali kuandaa sera na mipango mipya ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu na jinsi ya kuitekeleza na kufatilia utekelezaji wa mipango hiyo.

Alisema taarifa hizo zitakazopatikana kupitia zoezi hilo pia zitasaidia kujua wastani wa ongezeko la watu na hali ya uhamiaji mfano kutoka vijijini kuja mjini lakini hata waliotoka nje kuhamia na kuingia Tanzania.

"Sensa pia itatusaidia Serikali kufanya maamuzi kuhusu ugawaji wa rasilimali za Taifa na kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, maji, umeme, ujenzi wa miundombinu kulingana na idadi ya watu na mahitaji ya maeneo hayo" alisema Rais Samia.

“Ili Sensa iweze kukidhi mahitaji ya kufanikisha malengo yote hayo ni lazima ishirikishe watu wote. Zoezi hili litakuwa ni kwa watu wote waliolala na kuamkia siku ya Sensa kwenye nchi ya Tanzania,” alisema Rais Samia.

Alisema licha ya uwepo wa tozo za makazi, Serikali haikuwa na idadi sahihi ya nyumba na makazi, hivyo zoezi hilo litatoa ubora kwa kujua anuani za makazi, idadi ya majumba na aina za nyumba zilizopo.

Post a Comment

0 Comments