Ticker

6/recent/ticker-posts

COSOTA YABAINISHA MAENEO MANNE YA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA UTAMADUNI


***********************

Maeneo hayo yamebainishwa leo Aprili 04, 2022 Jijini Dodoma na Mwanasheria wa COSOTA Zephania Lyamuya alipokuwa akiwasilisha mada ya Usimamizi wa Hakimiliki na Maslahi ya Wasanii katika Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni kinachofanyika.

"COSOTA ingependa kushirikiana nanyi katika kukusanya Mirabaha, kutoa mwongozo wa usajili kwa wabunifu, kusaidia kupokea malalamiko ya uvunjifu wa Hakimiliki na kukusanya taarifa ya matumizi ya kazi za Muziki na Filamu katika Mabaa, Hotelini na Kumbi za Starehe hii itasaidia mgao wa mirabaha kuweza kuwafikia na wasanii ambao kazi zao zinachezwa Mikoani au Wilayani," alisema Lyamuya.

Akiendelea kuzungumza Mwanasheria huyo wa COSOTA alifafanua pamoja na kwamba Sheria ya Hakimiliki nchini inasema usajili wa kazi kwa ajili ya Hakimiliki siyo lazima sababu sheria inalinda bunifu zote bila kusajili, ila ni vyema kusajili kazi hizo ili mmiliki pamoja na wenye hakishiriki waweze kutambulika na kuweza kunufaika hata katika mgao wa mirabaha sababu mfumo wa mgao wa mirabaha unafanya mgao kulingana na taarifa zilizowasilishwa.

Post a Comment

0 Comments