Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA NA WADAU SHINYANGA, RC MJEMA APONGEZA HUDUMA YA AL - BARAKAH BANKING



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ( wa pili kulia) akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imewafuturisha Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wa Benki hiyo kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB imefanyika leo Jumatano Aprili 13,2022 katika ukumbi wa NSSF Mpya Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu, Watoto yatima na wateja na wadau wa Benki ya CRDB ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.


Akizungumza kwenye hafla hiyo ya kufuturisha, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa futari hiyo pamoja na kuendelea kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya jamii.

“Napenda kuushukuru Uongozi wa Benki ya CRDB kwa Iftari siku ya leo, Mwenyezi Mungu azidi kuwaongoza na kuangaza katika shughuli zenu. Niwapongeze Waislamu wote kwa kuendelea na funga katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kwani funga hii ni faradhi kama ilivyoelezwa katika Kitabu Kitukufu cha Quran”,amesema Mjema.

“Benki ya CRDB inatoa huduma zinazokidhi mahitaji ya jamii ikiwemo huduma ya Al- Barakah Banking ambayo ni mahsusi kwa ajili ya waumini wa dini ya Kiislamu. Nimeambiwa huduma hii ya Al- Barakah Banking inafuata sheria za Kiislamu ikiwemo mikopo ya bila riba”,amesema.

Amewaomba Waislamu ambao waliokuwa wanashindwa kutumia huduma ya Benki kwa sasa CRDB imezingatia mahitaji yao hivyo kuwasihi waende wakafungue akaunti ili fedha zao ziwe salama.


“Katika Mapinduzi ya Viwanda huduma za kibenki ni muhimu sana kwani awamu hii ya mapinduzi ya viwanda imejikita huduma kiganjani. Maana yake ni kwamba unapata huduma palepale ulipo. Kwa mfano leo ukiweka fedha zako benki unaweza kulipia huduma yoyote kwa kutumia simu yako ya mkononi ikiwemo kulipa bili za maji, Kununua LUKU, kulipa ada za watoto na huduma mbalimbali za kibenki”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga.


Amesema kwa wakati huu ni vyema wananchi wakatumia huduma za kibenki ambazo zinarahisisha upatikanaji na utumiaji wa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.


“Napenda kuupongeza uongozi wa Benki ya CRDB kwa kukubali maombi ya serikali ya kushusha riba ya mikopo ya sekta ya Kilimo hadi asilimia 9. Niwaombe wananchi tuchangamkie fursa hii ili kilimo chetu kiweze kuwa cha kisasa ambacho kitaongeza tija”,amesema Mjema.


Mjema ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022 huku akiwataka kuendelea kutoa ushirikiano katika zoezi la anwani za makazi.

Akitoa Salamu wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja na wadau wa benki hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi wa Benki ya CRDB, Bw. Pendason Philemon amesema Futari hiyo ni mwendelezo wa utamaduni wa Benki ya CRDB kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Kwetu Benki ya CRDB umekuwa ni utamaduni wetu kuandaa futari maalumu kwa ajili ya wateja wetu, wadau pamoja na wenzetu wenye uhitaji ambao wapo katika Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani. Futari hii ya leo ni mwendelezo wa utamaduni wetu kuungana na ndugu zetu wanaoshiriki mfungo kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu”,amesema Philemon.

Amesema sambasamba na kuandaa futari, Benki ya CRDB imekuwa ikishirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuainisha vituo vya kulelea watoto wenye uhitaji mkubwa na kuvipatia msaada wa futari ili kuwasaidia watoto na walezi wao kuitekeleza na kuikamilisha ibada ya swaumu kikamilifu.

“Katika futari hii ambayo ni ya pili kuifanya kipindi hiki baada ya kufanya mkoani Tanga, pia tumejumuika na watoto wetu wenye mahitaji maalumu ambao pamoja na kushiriki nao futari lakini pia tumewaandalia zawadi kidogo ya unga wa ngano, sabuni, mafuta ya kupikia na vitu vingine ambavyo vitawafaa katika kipindi hiki cha mfungo.Jambo hili litafanyika katika Kanda zote saba za Kibiashara za Benki ya CRDB”,amesema Philemon.

“Pamoja na ushiriki wetu katika mfungo wa Mwezi wa Ramadhani kupitia futari na misaada kwa wenye uhitaji, Benki yetu ya CRDB kwa kutambua uwepo wa mahitaji maalumu ya huduma za fedha kwa wenzetu wenye imani ya Kiislamu, tuliweza kukaa chini na kutengeneza bidhaa maalumu kwa ajili yao inayoitwa Al – Barakah ili kudhihirisha ni kiasi gani ambavyo Benki yetu inaishi katika kauli mbiu yake ya ‘Benki inayosikiliza mteja”,ameeleza.

Akielezea kuhusu Huduma mpya ya Al – Barakah Banking, Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kitengo cha Al – Barakah Banking, Thabit Galia amesema huduma hiyo ambayo haina riba na inayofuata misingi ya Sharia za Kiislamu inapatikana katika dirisha maalumu kwenye maeneo yote ambayo Benki ya CRDB inatoa huduma zake hivyo kuwaomba waumini wa dini ya Kiislamu kutumia huduma hiyo kwa ajili ya huduma za kifedha.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui wameamua kuandaa futari hiyo, baada ya Tanga ili kuonesha ni kiasi gani wanauthamini na kuupa thamani na heshima kubwa mkoa wa Shinyanga na kuthamini ushirikiano wa kibiashara unaotolewa na wakazi wa Shinyanga.

“Shughuli ni watu, isingekuwa na maana kama tungeandaa shughuli hii na kusiwepo na watu wa kushiriki nao. Tunawashukuru wote kwa kuitikia wito wa kujumuika nasi, mmetupa heshima kubwa.

Benki ya CRDB itaendelea kuwa tayari kushirikiana na wadau mbalimbali na jamii ya Watanzania siyo tu katika kipindi hiki ch Mwezi Mtukufu wa Ramadhani bali nyakati zote kama ambavyo tumekuwa tujinasibu na kauli mbiu yetu ya ‘Ulipo Tupo’”,amesema Pamui.

Naye, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amewashukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa Futari hiyo akieleza kuwa kipindi cha Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani ni wakati wa kujitafutia thawabu nyingi kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia ibada,ukarimu na upendo kwa ndugu,jamaa na marafiki na kutoa zaka na sadaka kwa wingi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa Jukwaa kuu wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga Jumatano Aprili 13,2022 katika ukumbi wa NSSF Mpya Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi wa Benki ya CRDB, Bw. Pendason Philemon akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi wa Benki ya CRDB, Bw. Pendason Philemon akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kitengo cha Al – Barakah Banking, Thabit Galia akielezea huduma ya Al Barakah Banking wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakiwa kwenye Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Watoto wenye uhitaji maalumu wakiwa kwenye Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ( wa pili kulia) akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kitengo cha Al – Barakah Banking, Thabit Galia na Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi wa Benki ya CRDB, Bw. Pendason Philemon (kulia) wakipata futari.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakiendelea kupata Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi wa Benki ya CRDB, Bw. Pendason Philemon akikabidhi zawadi kwa watoto wenye uhitaji kwa ajili ya Mfungo wa Ramadhani wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mtoto akiomba dua wakati Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi wa Benki ya CRDB, Bw. Pendason Philemon akikabidhi zawadi kwa watoto wenye uhitaji kwa ajili ya Mfungo wa Ramadhani wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa Benki ya CRDB na wadau baada ya kuwasili katika jengo la NSSF Mpya Mjini Shinyanga kwa ajili ya kushiriki  Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kushiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Post a Comment

0 Comments