Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI, UDSM WAINGIA MAKUBALIANO YA UJENZI WA KITUO CHA TAIFA CHA UKUZAJI WA VIUMBE MAJI BAHARINI KUNDUCHI

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Uvuvi,Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akiwa pamoja na wakisaini mkataba wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliofanyika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam, tarehe 22 Machi 2022. Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Uvuvi,Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akiwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye wakionesha mkataba waliosaini wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliofanyika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam,leo tarehe 22 Machi 2022. Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Uvuvi,Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliofanyika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam, tarehe 22 Machi 2022. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliofanyika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam, tarehe 22 Machi 2022. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam-UTAFITI Prof.Benadeta Killian akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliofanyika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam, tarehe 22 Machi 2022.Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Uvuvi,Dkt. Rashid Tamatamah akionesha kitu mbele ya wadau wa uvuvi katika eneo ambalo litatumika ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari katika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam leo tarehe 22 Machi 2022. Eneo ambalo litatumika ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari katika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam, leo tarehe 22 Machi 2022.

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Sekta ya Uvuvi imetoa ajira za moja kwa moja kwa wavuvi wapatao 195,435 na wakuzaji viumbe maji 30,064 wakati watu zaidi ya Milioni 4.5 wanajipatia kipato kutokana na shughuli mbalimbali katika minyororo ya thamani ikiwemo kuunda na kutengeneza boti, kushona nyavu, kuzalisha vifaranga na vyakula vya samaki, kutengeneza vizimba na biashara ya samaki.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Uvuvi,Dkt. Rashid Tamatamah katika hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya Kujenga, Kuanzisha na Kusimamia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Viumbe Maji bahari kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, uliofanyika Shule Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi - Kampasi ya Kunduchi, Dar es Salaam, tarehe 22 Machi 2022.

Amesema samaki huchangia takriban asilimia 30 ya protini inayotokana na Wanyama.

Aidha,amesema katika mwaka 2020/2021 jumla ya tani 483,756 zenye thamani ya Shillingi Trilioni 2.4 zilivunwa kutoka katika maji ya asili na tani 22,793.2 za mazao mbalimbali ya viumbe maji zenye thamani ya Shillingi Bilioni 166.38 zilizalishwa nchini.

Katika mwaka 2020, Sekta ya Uvuvi ilikua kwa asilimia 6.7 na kuchangia asilimia 1.71 ya Pato la Taifa.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema Chuo cha Uvuvi Kunduchi kilianzishwa kwa madhumuni ya kutoa elimu ya mafunzo ya uvuvi kwa minajili ya kupata wataalam na wagani wa kusimamia na kuendeleza Tasnia ya Uvuvi katika ngazi ya stashahada.

"UDSM kwa kuzingatia umuhimu wa tasnia ya sayansi za maji na uvuvi na hasa ukizingatia nia ya dhati ya Serikali ya Tanzania kuelekea kwenye Uchumi wa Buluu, mwaka 2020 UDSM ilichukua hatua ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya Sayansi Akua na Teknolojia Uvuvi na kuwa Shule Kuu inayojulikana kwa jina la Shule Kuu ya Sayansi Akua na Teknolojia ya Uvuvi (yaani School of Aquatic Sciences and Fisheries Technology – SoAF) inayoendesha shughuli zake mahali hapa kwa sasa". Amesema Prof.Anangisye

Amesema Asilimia kubwa ya wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, hususan Idara ya Uvuvi na wale wa Ufugaji Viumbe Maji, wamepata mafunzo yao kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments