WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya Kufungua Tamasha la Tanga Utalii Festival leo Jijini Tanga lililofanyika viwanja vya Urith Jijini humo ambalo liliandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa Tamasha hilo.
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Calvas Joseph akizungumza wakati wa Tamasha hilo.
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo kutoka kwa Bandari ya Tanga mara baada ya kutembelea banda lao.
WAZIRI wa Afya akipata maelekezo kwenye Banda la Benki ya Tanzania Comercial Benki wakati alipotembelea Banda lao.
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kutoka kwa Benki ya NMB wakati alipotembelea Banda lao.
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kushoto akipata maelezo kwenda Banda la Magoroto.
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki mshiriki kutoka Kivutio cha Utalii cha Magoroto kilichopo wilayani Muheza Aisiana Mero wakati alipofungua tamasha la Tanga Utalii Festival kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya.
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki mshiriki kutoka Kivutio cha Utalii cha Magoroto kilichopo wilayani Muheza Aisiana Mero wakati alipofungua tamasha la Tanga Utalii Festival kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo akifuatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akipokea tisheti wakati wa tamasha hilo.
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amefungua Tamasha la Tanga Utalii Festival huku akipigia chapuo vivutio vya utalii vilivyopo Jijini Tanga kwa kuwashauri watalii wanapokwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi waunganishe na Tanga kuona vuvutio vingine ikiwemo Beach nzuri,Visiwa vya Toten na Mapango ya Amboni.
Amesema pia Tamasha hilo la Tanga Utalii Festival litafungua fursa na kuongeza za kipato kwa wananchi wa mkoa wa Tanga na hivyo kuchochoe ukuaji wa uchumi kwa mkoa huo.
Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo leo wakati akifungua Tamasha la Tanga Utalii Festival ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza ambalo limeandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa na kushirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali.
Alisema upo umuhimu wa watalii wanapokwenda kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wanapomaliza badala ya kurudi uwanja wa ndege Kia watumia fursa hiyo kuja mkoani Tanga ili kuweza kuona vivutio adimi vilivyopo ikiwemo beach,visiwa na eneo la magoroto lenye vipepeo ambavyo havipatikani mahali pengine popote duniani.
Waziri Ummy alisema kwamba wanaweza kutumia jukwaa hilo ambalo kwa sasa litakuwa likifanyika kila mwaka kuhakaikisha wakuza fursa za ajira na uchumi kwa watu wa Tanga.
“Tunataka kulifanya Jiji la Tanga kuwa la Mahaba watu wa Mwanga na Same wanapokuja kutalii Mkomazi tuna maombi yetu watu wasiiishie mkomazi waje na Tanga tuwapeleke visiwa vya toten,beach Usongo Pangani ambapo kuna mchanga mzuri halafu waende Magoroto Muheza wanaona vipepeo”Alisema
Hata hivyo alisema jambo hilo ni nzuri na wao wataendelea kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Tanga huku akieleza kwamba Rais Samia Suluhu ametoa Milioni 500 kwa Jiji la Tanga kwa ajili ya kujenga Machinga Complex.
“Kwa kweli nimpongeza Dc Mgandilwa kwa kuandaa Tanga Utalii Festival ni jambo nzuri lengo lake ni kutaka kuonyesha utamaduni wa Tanga uzuri mila za Tanga nitoe wito kwa wakazi wa Tanga na nje ya Tanga kutembelea vivutio vilivyopo katika mkoa wa Tanga yakiwemo Mapango ya Amboni tunashukuru Mamlaka ya Ngorongoro wanayaboresha kila siku”Alisema
“Lakini Tanga pia tuna kisima cha maji Moto,Beach nzuri za kutembelea,kisiwa cha Toten tunaposema tunataka kulifanya Jiji la Tanga kuwa la mahabaa ukarimu na maendeleo ni kuonyesha mambo mazuri tulionayo ni jambo nzuri na sisi viongozi wenye asili ya Tanga tutakuunga mkono kuhakikisha tunaliboresha kila mwaka”Alisema
Awali akizungumza wakati wa tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema waliona watumie jukwaa hilo kutangaza fursa za utalii uliopo Jijini Tanga ikiwemo Visiwa,Mapango na Makaburi ya Shabani Robert kwani waliona bado hayajatangaza ipasavyo.
Alisema sambamba na kutangaza vivutio hivyo lakini pia kutangaza Utalii uliopo eneo la Magoroto wilayani Muheza ikiwemo na baadhi ya samaki silikant huku akieleza kuanzishwa kwa tamasha hilo ni kutangaza vivutio vilivyopo kwa wadau.
Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo lengine ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo na kuhamasisha sensa ya watu na makazi kwa wananachi na wanaamini tamasha hili litakuwa endelevu lengo ni kutangaza utalii .
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo alisema wamekuja kumuunga mkono Waziri Ummy kutokana na kazi nzuri anayoifanya nchi na jimbo na wilaya ya Same umekuja kufanya kazi kubwa na nzuri hivyo pia niwahamasisha wananchi kutembelea vuvutio vya utalii vilivyopo nchini.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya Alisema wao kama wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wameona kuna umuhimu wa kuja kuunga mkono tamasha hilo.
0 Comments