Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MULAMULA AWASILI SAUDI ARABIA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akimsikiliza Bw. Hussyan Alrashid , Mkurugenzi wa Idara ya Afrika - Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia (katikati) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa jjini Riyadh alipompokea Mhe. Waziri Mulamula alipowasili nchini Saudi Arabia
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na mwenyeji wake kulia akizungumza alipowasili katika uwanja wa ndege wa jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kuanza ziara ya kikazi nchini humo, wa kushoto kwa Mhe. Waziri ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na mwenyeji wake kulia akizungumza alipowasili katika uwanja wa ndege wa jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kuanza ziara ya kikazi nchini humo, wa kushoto kwa Mhe. Waziri ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) katika kikao cha paamoja na timu aliyoambatana nayo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kujipanga kwa pamoja wakati wa ziara ya kikazi nchini humo mara baada ya kuwasili. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akimsikiliza.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (wa pili kutoka kulia) akiwa na maafisa wengine wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia hayupo pichani wakati wa kikao cha pamoja kuhusu ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania nchini Saudi Arabia mara baada ya kuwasili nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (katikati) akizungumza katika kikao cha kujipanga huku Waizri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto ) akimsikiliza na kulia kwa Mhe. Balozi ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini (TCCIA )Bw. Pal Koyi akiandika yanayojiri.


*************************


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 9 hadi 12 Machi 2022.


Ziara hiyo inafuatia mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021.


Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara.


Akiwa nchini Saudi Arabia Mhe. Waziri Mulamula anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi, viongozi wengine wanaosimamia sekta za sekta za Mifugo na Utalii na wafanyabiashara na wenye viwanda wa Saudi Arabia.

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania mjini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah..


Balozi Mulamula na ujumbe wake watarejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

Post a Comment

0 Comments