Ticker

6/recent/ticker-posts

TET YAWATAKA WATAALAMU WA UANDISHI WA VITABU VYA KIADA KUTANGULIZA UZALENDO


************************

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba amewataka wataalamu wa uandishi wa vitabu vya kiada vya kidato cha kwanza hadi cha sita vya masomo ya Biashara, Sanaa, Lugha ya Kichina, Maarifa ya nyumbani, Hisabati, Kiarabu na Kifaransa kutanguliza uzalendo na kuifanya kazi kwa umakini kwani kazi hiyo ina masalahi mapana ya Taifa.

Ameyasema hayo, leo tarehe 23/03/2022 alipowatembelea watalaamu hao katika eneo la kazi ya uandishi wa vitabu inayofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Morogoro na Taasisi ya Elimu ya watu wazima Mjini Morogoro, ambapo amesema kuwa bila kuifanya kazi kwa umakini na kuzingatia maudhui ya vitabu yanaendana na watumiaji husika .

“Nawaomba sana muwe makini na wazalendo katika kazi hii ya uandishi wa vitabu ili kuwezesha malengo yake kukamilika vizuri”amesema Dkt.Aneth.

Aidha amewashukuru watalaamu hao kwa kuendelea na kazi hiyo na kuwaeleza kuwa wanatarajia kazi hiyo ikamilike kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake mratibu wa zoezi la uandishi wa vitabu hivyo, Bwana.Jonathan Paskali amesema jumla ya watalaamu 237 kutoka katika vyuo vikuu ,vyuo vya ualimu na shule za sekondari nchini wanashiriki katika zoezi hilo.

Aidha Paskali amesema kuwa jumla ya aina 40 za vitabu vya masomo hayo vinatarajiwa kuandikwa.

Post a Comment

0 Comments