Ticker

6/recent/ticker-posts

SHUWASA YAZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)Mwamvua Jilumbi, akizindua Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.
Muonekano wa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA


Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imezindua kitabu cha mkataba wa huduma kwa wateja, ambao utakuwa kiungo kati ya Mteja na Mamlaka kwa kuzitambua haki na wajibu kwa pande zote mbili.


Uzinduzi huo wa mkataba wa huduma kwa wateja umefanyika leo March 18,2022 ikiwa ni sehemu ya katika Maadhimisho Wiki ya Maji iliyoanza tarehe 16 - 22, 3.2022 wakati wa Warsha ya wadau wa Maji iliyohudhuriwa na Madiwani, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa serikali za mitaa,Kamati ya Amani ya Wilaya na wadau wa Maji iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.


Afisa Uhusiano na Umma kutoka SHUWASA Nsianel Gerald, amesema mwaka 2021 walifanya kikao na wadau cha kupitia Rasimu ya Mkataba kwa pamoja na kupata maoni ya kuboresha mkataba wa huduma kwa wateja na kuwasilishwa kwa mapitio kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Usimamizi wa huduma za Nishati na Maji- EWURA na mrejesho umeshakamilika na leo uzinduzi rasmi umefanyika na zoezi la ugawaji wa kitabu hicho ni endelevu kwa wadau.


“Mkataba huu wa huduma kwa Mteja utatoa chachu ya utendaji kazi kwa watumishi wa Mamlaka na utasaidia kuendelea kutoa huduma bora ya majisafi na salama katika Manispaa yetu na Miji ya Tinde Didia na Iselamagazi”, amesema Gerald.


Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola, akitoa taarifa ya utendaji wa shughuli za Mamlaka , amewataka wananchi wa Shinyanga kuvitunza vyanzo vya maji hasa bwawa la Ning’wa lililopo Kata Chibe Manispaa ya Shinyanga kulitunza ili liendelee kuhudumia vizazi na vizazi vijavyo.


Amesisitiza kuwa kutunzwa kwa bwawa la maji la Ning’wa, ni muhimu kwani tatizo la maji kutoka Mtandao wa Ziwa Victoria linapojitokeza hulazimika kutumia chanzo hicho hivyo kuitaka jamii iache kufanya shughuli za kibinadamu kama vile kilimo kwenye vyanzo vya maji ili visitoweke au kupungua kina.


Ameitaja miradi ambayo mamlaka hiyo inaitekeleza na kutarajia kuitekeleza kwa kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, ukiwemo mradi wa maji wa Tinde, Didia hadi Shelui unaotekelezwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na SHUWASA, KASHWASA na RUWASA Mkoa wa Shinyanga ya maji wenye gharama ya Sh. bilioni 12.


Amesema pia katika fedha za mapambano dhidi ya UVIKO-19 Sh. milioni 469.8 ambazo walizipokea kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, watazielekeza kwenye maeneo mengine yenye uhitaji wa maji ambayo ni Didia, Iselamagazi na kuongeza mtandao wa maji katika Kata za Kolandoto, Ibadakuli, Ibinzamata, Chibe Mwalugoye, na Kizumbi.


Amesema katika fedha zingine Sh. Milioni 500 kutoka Bajeti kuu ya Serikali katika mwaka wa fedha (2021-2022) wataekeleza fedha hizo Sh. milioni 300 kupeleka maji safi na salama katika kijiji cha Bugayambelele, na fedha zingine zilizosalia zitatumika kununua vifaa kwa ajili ya maunganisho ya maji.


Pia amesema kupitia mfuko wa maji kuna kiasi cha fedha Sh. milioni 800 ambazo zitatumika kupeleka mtandao wa maji katika maeneo ambayo ni mapya, ambapo kiasi cha Sh. milioni 450 zitatumika kujenga mtandao wa maji katika mji mdogo wa Didia.


Katika hatua nyingine amesema kupitia fedha za Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) wanatarajia kupokea kiasi cha fedha Sh. bilioni 190, fedha ambazo zitasaidia kumaliza tatizo la huduma ya maji katika maeneo yote ya Shinyanga.


Amesema, Mamlaka hiyo pia watajenga mtandao wa maji taka kutoka viwandani, pamoja na mtambo wa kuchakata maji taka.


Naye Mwanasheria wa SHUWASA Happy Richard, akisoma vifungu vya sheria kuhusu uharibifu wa vyanzo vya maji na miundombinu, kwa mujibu wa sheria ya maji na usafi wa mazingira ya mwaka 2019, alisema ufanyaji wa shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji faini yake ni Sh. 50,000 hadi Milioni Moja au kifungo cha Mwezi Mmoja hadi Mitatu au kupewa adhabu zote kwa pamoja kulipa faini na kifungo juu.


Amesema kwa upande wa uchafuzi wa maji faini yake ni Sh. milioni moja hadi 10, au kifungo cha miezi Sita hadi miaka miwili au vyote kwa pamoja, na kuwasihi wananchi waache tabia ya uharibifu wa vyanzo vya maji na miundombinu, ikiwamo kuacha uchomaji wa mabomba, na kujenga nyumba juu ya mabomba ya maji hasa ya milimita 150 hali ambayo ni hatari.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Mwamvua Jilumbi, akizungumza wakati wa kufungua Warsha hiyo, amewataka wadau hao wa maji ambao wamehudhuria warsha, wakatoe elimu vyema kwa wananchi juu ya kuacha kuharibu vyanzo vya maji na miundombinu ya maji, ili waendelee kupata huduma ya maji safi na salama.


Pia, amewataka wananchi wa Shinyanga kuwa katika wiki hii ya maadhimisho ya maji duniani, kwa wale ambao wana madeni na walikatiwa maji, wachangamkie fursa hiyo ya kulipa madeni yao kwa sabau sababu hakutakuwa na faini ya kurejesha huduma hadi mwisho wa mwezi huu.


Kwa kupitia kauli mbiu ya wiki ya maji mwaka huu isemayo “Maji chini ya Ardhi hazina isiyo onekana kwa maendeleo endelevu”.basi tuizingatie kwa umoja wetu.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akizungumza kwenye Warsha na uzinduzi wa Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja leo Ijumaa Machi 18,2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandis Yusuph Katopola akizungumza kwenye Warsha hiyo ya wadau wa Maji na uzinduzi wa Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majsafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandis Yusuph Katopola akizungumza kwenye Warsha hiyo ya wadau wa Maji na uzinduzi wa Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.
Afisa Uhusiano na Umma kutoka SHUWASA Nsianel Gerald, akielezea uzinduzi wa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.
Mwanasheria wa SHUWASA Happy Richard akifafanua sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019 namna inavyo mwajibisha mtu ambaye ana haribu vyanzo vya maji na miundombinu ya maji.
Wadau wa maji wakiwa kwenye Warsha hiyo ya SHUWASA na uzinduzi wa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.
Mdau wa Maji Zengo Mikomangwa akichangia hoja wakati wa Majadiliano kwenye Warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Solomon Najulwa, akichangia hoja wakati wa Majadiliano kwenye Warsha hiyo.
Askofu Josephat Musira wa Kanisa la TMRC Ndembezi, akichangia hoja wakati wa Majadiliano kwenye Warsha hiyo.
Shekhe Masoud Ramadhani akichangia akichangia hoja wakati wa Majadiliano kwenye Warsha hiyo.
Diwani wa Chibe John Kisandu, akichangia hoja kwenye Warsha hiyo, hasa Mada ya uharibifu wa vyanzo vya maji, kwa sababu chanzo kikubwa cha maji Bwawa la Ning'wa lipo katika eneo lake.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Wadau wakiendelea na Warsha hiyo.
Watumishi wa SHUWASA wakiwa kwenye Warsha hiyo ya wadua wa maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akizindua Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi (kulia) akizindua Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akikabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja kwa kundi la Madiwani, ambao waliwakilishwa na Diwani wa Ndala Mhe. Zamda Shabani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akiendelea kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja.
Zoezi la kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja likiendelea kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye Warsha hiyo.
Zoezi la kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja likiendelea kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye Warsha hiyo.
Zoezi la kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja likiendelea kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye Warsha hiyo.
Zoezi la kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja likiendelea kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye Warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akikabidhi Kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja kwa Katibu wa Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson
Zoezi la kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja likiendelea kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye Warsha hiyo.
Zoezi la kukabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja likiendelea kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye Warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akikabidhi kitabu cha Mkataba wa huduma kwa mteja kwa waandishi wa habari, ambao waliwakilishwa na Mwandishi wa ITV Frank Mshana.

Post a Comment

0 Comments