****************
Viongozi wakuu wa nchi usiku wa Machi 8, 2022, wamekuwa miongoni mwa watanzania walioadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kushiriki Tamasha la aina yake la Orange Concert.
Tamasha hilo lililoenzi ubunifu wa sekta za sanaa na michezo ambapo taasisi ya wasanii ya Dadahood na Baraza la Michezo Tanzani ziliungana pamoja na mambo mengine kutumia sanaa kuwachangia Twiga Stars, limetia fora katika mwaka wake wa kwanza tu.
Kiongozi wa kwanza kufuatilia alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alituma ujumbe wa kuchangia milioni 10 kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Baada ya muda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye kupitia kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Mchemba, akapiga simu na kuchangia milioni 15.
0 Comments