Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MWINYI ATUNUKIWA TUZO YA KISWAHILI NA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.


***********************

Na. John Mapepele

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, leo Machi 18, 2022 imemtunukia tuzo ya heshima ya Kiswahili, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Pili la Idhaa ya Kiswahili jijini Arusha.

Tuzo hiyo ya heshima ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili iliyokabidhiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Serikali.

Kwa upande wake Mhe. Rais Mwinyi ameishukuru Serikali kwa kumtunukia tuzo hiyo na kueleza kuwa atampatia ari zaidi ya kuendelea kukitangaza Kiswahili duniani.

Aidha, ametoa wito kwa Kamati ya Maandalizi kufikiria kufanyia Kongamano la tatu mwakani Zanzibar ili kuleta maana zaidi ya kueneza na kuendeleza Kiswahili.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na takribani washiriki 200 kutoka idhaa mbalimbali za Kiswahili duniani.

Akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameiomba Serikali kuweka vituo vya Utamaduni kwenye Balozi za Tanzania nje ya nchi ili kukuza na kuendeleza Kiswahili.

Katika Kongamano hili Mhe. Rais Mwinyi alipata fursa ya kuzindua mfumo wa kufundisha Kiswahili pamoja na kutoa vyeti vya kuwatambua washiriki na wadhamini.

Kongamano hili limerushwa mbashara na TBC, ZBC na vituo kadhaa vya Redio na televisheni.

Post a Comment

0 Comments