Baadhi ya wageni walioendelea kutembelea Banda la NEMC wakiendelea kupata elimu jinsi usimamizi na utunzaji wa Mazingira nchini Tanzania unavyofanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.Miongoni mwa wageni waliotembea banda la NEMC nchini Qatar ni mke wa Balozi wa Tanzania (katikati aliyevaa mtandio kichwani) Bi. Safia Mahadhi ambaye ameipongeza NEMC kwa kushiriki maonesho hayo na kuwashauri kuwa yale mazuri waliyojifunza wayapeleke nchini Tanzania kwa lengo la kuboresha mazingira na fursa za uwekezaji nchini.Leo tarehe tarehe 13/3/2022 Banda la NEMC nchini Qatar lilitembelewa na balozi wa Tanzania ( katikati) Mh. Dkt. Mahadh Maalim pamoja na balozi wa Kenya (wa pili kulia) nchini Qatar Mh. Paddy Ahenda wamepongeza NEMC kwa kushiriki maonesho makubwa ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira na kuwashauri waendeee kutumia fursa kama hizi ili kutoa elimu na kuitangaza nchi kupitia hifadhi na utunzaji wa Mazingira. Bodi ya Kahawa yaendelea kuvutia wanunuzi wa Kahawa nchini Tanzania kupitia maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar.Wizara ya Mambo ya Nje yaendelea kung'ara maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar.
Mteja akisikilizwa kwenye Banda la NEMC nchini Qatar Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) wametembelea Kampuni ya Elite Paper Recruiting nchini Qatar inayojishughulisha na urejerezaji wa taka za karatasi. Kampuni hii inakusanya taka za karatasi toka maeneo mbalimbali nchini Qatar na kuzirejereza ili kupata bidhaa za karatasi. Hivyo, Kampuni hii inasaidia kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza bidhaa za karatasi hivyo inasaidia kutunza Mazingira hususani katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi. Kampuni hii inasambaza bidhaa zake katika mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania hivyo ni fursa nzuri kwa Tanzania kupitia NEMC kushirikiana nao kuanzisha viwanda vya kurejereza taka za karatasi kwa lengo la kupunguza uchafuzi wa Mazingira na kuongeza fursa za ajira nchini.
0 Comments