Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII YATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUTUNZA MAZINGIRA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI


************************

Na.Dominic Haule

Katika kuhakisha Wanakabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya nchi Jamii imetakiwa kuwa na Utamaduni wa kutunza Mazingira katika jamii ikiwemo kuwafundisha Vijana na hasa watoto Maswala ya Utunzaji wa Mazingira ili kuhakikisha Mazingira yana kuwa katika hali nzuri katika kizazi Cha Leo na Cha kesho.

Hayo amesema Jijini Dar es salaam Bi .Nyendo Kinyonga ,Mtaalamu wa Elimu, Mazingira na Ulinzi wa Mtoto, wakati wa Uzinduzi wa Soma na mti katika kanda ya Ubungo pamoja na kushiki zoezi la kufanya Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya Bahari iliyo anadaliwa na Taasisi inayo jihusisha na Utunzaji wa Mazingira HUDEFO chini ya Mkurugezi wa taasisi hiyo Bi. Sarah Pima.

Amesema kuwa Ili mazingira yawe salama ni lazima kila mmoja aweze kuyafanya mazingira yawe endelevu na kufikia malengo yaliyo weka na Dunia ikiwa lengo kuleta tija katika kizazi cha leo na cha baadae..

Bi Kinyonda ambae pia mdau wa Mzingira amesema kuwa jamii inapo chukua hatua ya kutunza Mazingira hasa katika kufundisha Vijana juu ya Utunzaji wa mazingira unakuwa wa uendelevu wakutunza Mazingira hivyo basi Kila Mtu awajibike juu ya Utunzaji na kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya nchi .

Hata hivyo Bi Kinyonga ameitaka jamii hasa Wazazi na walezi waweze chukua jukumu la kuwajengea uwezo wa Kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi Kupitia kuwa kuhamasisha watu Maswala mazima ya kutunza ikiwa lengo kuadhimisha na kuendeleza Mazingira yanayo wazunguka .

Aidha amezitaka Taasisi mbalimbali katika jamii ziweze Kushiriki katika Utunzaji wa Mazingira na Kila Mara kuwa mstali mbele juu kutoa Elimu kwa jamii ili waweze kutunza Mazingira yanayo wazunguka badala ya kufanya Uchafunzi amabao utachochea kuleta asali na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Katika hatuta nyingine amewataka wanawake kuwa wanapo endelea kusherekea Siku ya Wanawake Duniani Wanawake wawe kipao mbele ya kutunza Mazingira yanayo wazunguka ili Mazingira yaweze kuwalinda hivyo Kilamoja anapaswa kutoa na fasi ya kufanya maamuzi juu ya Maswala ya Uchafunzi Mabadiliko ya Tabia ya nchi hasa katika sekta Mazingira kwa kua wao wanafasi kubwa ya kupeleka ujumbe wa elimu ya mazingira na ikaenda na kuja na matokeo chanya .

Zoezi hilo la Uzinduzi wa Soma na mti katika kanda ya Ubungo pamoja na kushiki zoezi la kufanya Usafi wa Mazingira katika Maeneo ya Bahari iliyo anadaliwa na Taasisi inayo jihusisha na Utunzaji wa Mazingira HUDEFO ilishirikisha wadau tofauti ikiwemo Waziri mwenye zamana ya Dokta Seleman Jafo Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na wadau wengine kutoka taasisi mbali mbali zinazo fanya shughuli ya Mazingira.

Post a Comment

0 Comments