Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida,Eva Mosha akizungumza kwenye kongamano la siku ya Taaluma na kujadili mbinu za kuongeza ufaulu kwa wanafunzi lililofanyika wilayani Ikungi hivi karibuni kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya akitoa taarifa kwenye kongamano hilo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi, Grace Kasege akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Afisa Elimu Mstaafu wa Mkoa wa Singida, Hamis Maulid akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Taswira ya kongamano hilo.
Burudani zikitolewa.
Burudani zikitolewa kwenye kongamano hilo.
Afisa Mahusiano ya Jamii wa Kampuni ya Shanta, Mukein Habib akizungumza kwenye kongamano hilo.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC Tawi la Singida Olairiuani Elirehema akizungumza na wadau na wananchi kwenye kongamano hilo.
Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Singida Musa Walwa akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Burudani ikiendelea.
Makamu Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Stephen Mtyana akichangia jambo.
Madiwani wa Viti Maalumu wa Halmashauri hiyo wakiwa kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Diwani Margaret Chima (Ikungi) na Theresia Masingisa.
Zawadi zikitolewa kwa waliofanya vizuri.
Vyeti vikitolewa kwa washindi.
Vyeti kwa washindi vikitolewa na mgeni rasmi.
Zawadi zikitolewa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ikungi wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wadau wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Pallot Daud Bulali akielezea mafanikio ya shule hiyo kitaaluma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Unyahati, akielezea mafanikio ya shule hiyo.
*************************
Na Dotto Mwaibale, Singida
HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imezidi kung'ara kitaaluma kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya wadau wote wa elimu katika wilaya hiyo.
Hayo yalibainika kwenye kongamano la siku ya Taaluma na kujadili mbinu za kuongeza ufaulu kwa wanafunzi lililofanyika wilayani humo hivi karibuni.
Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida,Eva Mosha alisema mafanikio hayo ya kukua kwa taaluma wilayani humo na Mkoa wa Singida kwa ujumla yametokana na ushirikiano uliopo baina ya wadau wote wa elimu.
"Ushirikiano huu uliopo ni muhimu sana kuuendeleza ili halmshauri yetu ya Ikungi na mkoa kwa ujumla uwe juu kitaaluma katika shule zetu zote kuanzia za msingi na Sekondari" alisema.
Aidha Mosha alisema mbinu nyingine ambayo ni kubwa ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi mashuleni ni suala la chakula kwa wanafunzi wakiwa shuleni.
"Wanafunzi kupata chakula shuleni ni jambo la muhumu hivyo nawaomba wazazi kujitokeza kusaidia kupatikana kwa chakula mashuleni" alisema Mosha.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya akitoa taarifa kwenye kongamano hilo alisema kukosekana kwa matundu ya vyoo kwenye baadhi ya shule kunaathiri utoaji wa elimu na kunaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa ya matumbo.
Akizungumzia maendeleo ya taaluma alisema wilayahiyo imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka na kuwa katika kipindi cha miaka mitatu imepata mafanikioya kuongeza udahili wa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza.
Alitaja mafanikio mengine kuwa ni ongezeko la miundombinu na samani ambapo kwa mwaka 2021/2022 idara ya elimu ilipokea fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo kupitia fedha za mapambano ya UVIKO 19, LANES na EP4R ambapo waliweza kujenga vyumba vya madarasa na miundombinu mingine kwa gharama ya Sh. 1,721,872,000.85.
Alitaja baadhi ya changamoto walizonazo ni upungufu wa walimu kwa shule za msing na upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati kwa shule za sekondari, upungufu wa majengo kama vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo na miundombinu mingine ya shul na ukosefu wa rasilimali za ufuatiliaji kama vile fedha, mafuta, magari na shajala.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Haika Masawe akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, alisema wataendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu na kuona wilaya hiyo inaendelea kuwa juu kitaaluma kwa kuwa wananchi wa Ikungi ni wapenda elimu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akizungumza kwenye kongamano hilo alisema ili kuinua michezo katika wilaya hiyo alifanya jitihada za kujengwa kwa kiwanja cha michezo ambapo Serikali imetoa Sh.400 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja hicho kitakacho jengwa Shule ya Sekondari ya Unyahati kama alivyoshauri.
Aidha katika hatua nyingine Mtaturu ameiomba halmashauri hiyo iwapo zitatokea nafasi za ajira za walimu kutoa kipaumbele kwa walimu waanzilishi wa Shule Shikizi ambapo sasa zimesajiliwa kuwa shule za msingi kutokana na kazi kubwa ya kizalendo walioifanya walimu hao.
Alizitaja baadhiya shule hizo kuwa ni Shule ya Msingi IShingisha, Sindikwa na Bunku.
Mwalimu Daud Bulali wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Palloti ambayo ilifanya vizuri kiwilaya alisema siri kubwa ya ushindi huo ni ushirikiano walionao baina ya walimu, uongozi wa shule na wanafunzi.
Alisema shule hiyo mwaka jana ilikuwa ya kwanza kiwilaya na mkoa walikuwa na wanafunzi 92 waliofanya mtihani ambapo divisheni moja walikuwa 61, divisheni mbili walikuwa 30 na divisheni tatu alikuwa mmoja na kuwa hawakuwa na divisheni nne wala ziro.
"Siri kubwa ya ushindi huu ni walimu kujituma kufundisha na wanafunzi kujengwa katika misingi ya kile wanachofundishwa" alisema Bulali.
Katika kongamano hilo Wanafunzi waliofanya vizuri pamoja na walimu wao walizawadiwa zawadi mbalimbali vikiwemo vyeti na ngao lakini kwa kwa Shule ya Sekondari Sepuka na Mpugizi ambazo hazikufanya vizuri zilizawadiwa zawadi ya vifago.
0 Comments