Afisa Masoko (TBS) Bw. Mussa Luhombero akitoa elimu kuhusu majukumu ya TBS, umuhimu wa kusoma maelezo yapatikanayo kwenye kifungashio, umuhimu wa kuangalia mwisho wa muda wa matumizi katika bidhaa na namna ya kutambua alama ya ubora ya TBS kwa bidhaa zilizothibitisha kwa wanafunzi wa shule za Sekondari za Nkasi na Nkomolo wakati wa kampeni ya uelimishaji umma wilayani Nkasi - Rukwa
Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bw. Emmanuel Mushi akitoa elimu ya jinsi ya kutambua bidhaa zilizothibitishwa,umuhimu wa kusoma taarifa za mzalishaji na muda wa mwisho wa matumizi ya bidhaa husika kwa wananchi na wafanyabiara wa soko la Sofia wilayani Kasulu-Kigoma wakati wa kampeni ya elimu kwa umma.
*************************
Wananchi 23,745 kati yao 18,645 wakiwa ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika wilaya za Kasulu, Mlele na Nkasi wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) sambamba na kuwahamasisha wafanyabiashara kusajili maduka ya chakula na vipodozi.
Wananchi hao walipatiwa elimu hiyo kupitia kampeni ya kutoa elimu kwa umma iliyoendeshwa na shirika kwenye wilaya hizo ambayo imelizika mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo ya elimu kwa umma ilifanyika katika maeneo mbalimbali kwenye ya shule za msingi na sekondari, masoko, stendi, minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo ubora wa bidhaa.
Afisa Masoko wa TBS, Bw Mussa Luhombero aliwakumbusha wananchi kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee, bali ni ya Taifa kwa ujumla.
“Kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 23,645 kati yao wanafunzi wa shule za msingi na sekondari 18,764 na wananchi 5100,” Alisema Luhombero
Luhombero aliwafafanulia wanafunzi pamoja na walimu umuhimu wa viwango katika maisha yao ya kila siku vilevile kuwafahamisha fursa ya huduma bure kwa wajasiriamali wadogo na aliwaasa kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha ubora katika jamii wanazoishi.
Vilevile aliwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi wanapokutana na bidhaa zilizokwisha muda wake au wanapotilia shaka bidhaa yoyote katika soko au zilizopigwa marufuku kama vile nguo za ndani za mitumba, mafuta ya breki dot 3 na baadhi ya vipodozi.
Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kufuatilia taratibu sahihi za usajili wa bidhaa au majengo kupitia mawasiliano waliyopewa pamoja na kutembelea ofisi ya TBS iliyopo karibu au kupiga katika kituo cha huduma kwa wateja.
0 Comments