Ticker

6/recent/ticker-posts

CHAMA, KAGERE WAIWEZESHA SIMBA SC KUICHAPA DODOMA JIJI


*************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeiadhibu timu ya Dodoma Jiji kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara NBC Premier League na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu.

Katika mchezo huo tulishuhudia timu zote zikienda mapumziko zikiwa hazijapata bao licha ya kosa kosa kibao kutokea kwa timu zote mbili.

Kipindi cha pili kilianza Simba Sc kuendelea kulisakama lango la Dodoma Jiji kutafuta bao la kuongoza hivyo wakafanikiwa kupata penati mara baada ya mchezaji wa Dodoma Jiji kuunawa mpira ndani ya boksi.

Mkwaju wa penati ulienda kupigwa na Kiungo Mshambuliaji wao Clautos Chama na kufanikiwa kuiwezesha timu yake kuongoza kwa bao la kwanza dakika ya 57.

Dodoma Jiji Fc nao walianza kutafuta bao la kusawazisha kwa kushambulia lango la Simba Sc bila mafanikio mwisho Simba Sc ilipata nafasi na kuweza kuongeza bao la pili kupitia kwa Mshambuliaji wao Meddie Kagere dakika ya 75 ya mchezo.

Post a Comment

0 Comments