Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, YAICHAPA MTIBWA PALE PALE MANUNGU



**************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imeendelea kutoa dozi ligi ya NBC ambapo leo imeitembezea kichapo timu ya Mtibwa Sugar kwenye dimba la Manungu mkoani Morogoro.

Mabao ya Yanga Sc yamewekwa kimyani na mshambuliaji wao Said Ntibazokiza pamoja na Fiston Mayele ambaye mpaka sasa ana magoli 7 kwenye ligi.

Yanga sasa itaendelea kukaa kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya mpinzani wake Simba Sc.

Post a Comment

0 Comments