WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa,akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo za walimu za ubora wa taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kidato cha nne na kidato cha sita kwa mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara. katibu mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzanaia (CWT ),Mwalimu, Deus Seif,akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo za walimu za ubora wa taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kidato cha nne na kidato cha sita kwa mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara. Sehemu ya walimu na wanafunzi walioshiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa (hayupo pichani) katika hafla ya utoaji tuzo za walimu za ubora wa taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kidato cha nne na kidato cha sita kwa mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara.
**************************
Na Zena Mohamed,Dodoma. WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita(TAMISEMI),Innocent Bashungwa amewataka wakuu wa shule zote nchini kuwa na utaratibu wa kuandaa motisha kwa walimu na wanafunzi ili kujenga ari ya ushindani na kuwa viungo kati ya jamii na viongozi wanao wazunguka kwa kuishi kwa ushirikiano ambao utawasaidia katika kutekeleza kwa ufasaha miradi mbalimbali ya serikali katika jamii.
WAZIRI Bashungwa alisema hayo jijini hapa leo katika hafla ya utoaji tuzo za walimu za ubora wa taaluma kwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kidato cha nne na kidato cha sita kwa mwaka 2021 kwa mikoa 26 ya Tanzania bara. Amesema ili kufikia malengo ya serikali ni lazima kusimamia miradi yote kwa ufasaha na iendane na thamani ya fedha, na mali za shule zitunzwe kwa ufasaha ili ziweze kutumika na vizazi vijavyo.
"Natoa maagizo kwa wakuu wote wa shule nchini kuhakikisha kwamba wanasimamia sheria, miongozo na taratibu katika sekta ya elimu, kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, pamoja na kutunza majengo ili yatumike hata katika vizazi vijavyo,"amesema Bashungwa. Wapo baadhi yenu hawana mahusiano mazuri na jamii hivyo hukwamisha utekeleaji wa baadhi ya shughuli za serikali hasa miradi mnapokuwa na mahusiano mazuri na viongozi katika jamii hii pia inarahisisha katika utekelezaji na hata utunzaji wa majengo ya serikali,”amesema
Kwa upande wake Kaimu rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu, Dina Mathamani amesema wao kama walimu wameona umuhimu wa kutoa tuzo na pongezi kwa walimu waliofanya vizuri na kuwafanikisha wanafunzi kufaulu vizuri.
“Ufaulu unaendelea kupanda siku hadi siku taaluma zinapanda na mazingira ya walimu yataendelea kuboreshwa na niahidi kwa niaba ya Chama cha walimu tutafanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka ili tupate wataalamu katika sekta mbalimbali”amesema Mwl.Mathamani.
Naye katibu mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzanaia (CWT ),Mwalimu, Deus Seif amesema Chama kinatambua jitihada kubwa zinazofanywa na serikali katika kuboresha maisha ya watanzania wakiwemo walimu.
“Miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, (SGR) lakini katika Sekta ya elimu yapo mambo kadhaa ambayo serikali imeyafanya ikiwemo ongezeko la miundo mbinu na samani ,upandishwaji wa madaraja na urekebishwaji wa mishahara kwa walimu, pamoja na malimbikizo ya madeni yasiyo ya mishahara”amesema Deus.
Hata hivyo amesema pamoja na jitihada za Serikali lakini bado walimu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa nyumba za walimu, madai mbalimbali ya walimu bado yapo katika halmashauri pamoja na ajira kwa walimu.
0 Comments