Ticker

6/recent/ticker-posts

TWCC YAHIMIZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUSHIRIKI KUWANIA TUZO ZA VIWANDA 2022



*************

Dar es salaam.

NA EMMANUEL KAWAU

Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania TWCC kimewahimiza Wanawake Wajasiriamali kushiriki kuwania Tuzo za Viwanda 2022 zinazotarajiwa kutolewa Machi 9 Mwaka huu kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika uchumi wa Taifa kupitia viwanda na biashara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa TWCC Mercy Sila amesema lengo Kuu la Tuzo hizo ni kutambua na kuheshimu mafanikio ya Wanawake katika Sekta ya Viwanda na Biashara pamoja na kuwahamasisha Wanawake kuwekeza na kujihusisha na Shughuli za Uzalishaji.

Hata hivyo. Mercy Sila amesema Tuzo hizo zitaambatana na wiki ya Viwanda na Maonyesho ya Bidhaa zinazo zalishwa na Wanawake wajasiriamali yatakayofanyika Machi 3 Hadi 8 2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

"Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini na kutoa mikopo kuanzia ngazi ya halmashauri kwa wanawake na vijana" Alisema Bi. Merce Sila.

Mchakato wa Upatikanaji wa Washindi wa Tuzo hizo umeanza Tangu Januari 29 2022 ambapo TWCC imewahimiza Wanawake wajasiriamali kujisajili na kujaza fomu za ushiriki wa Tuzo hizo ambazo fomu hizo zinapatokana katika Ofisi za TWCC Nchini, Ofisi za Mikoa pamoja na Ofisi za Shirika la Viwanda vidogo SIDO Mikoa yote.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa TRADEMARK Nchini Tanzania Monica Hangi ambao ndio Wadhamini wa Tuzo hizo amesema katika Sekta ya Biashara na Viwanda wapo wanawake wengi waliojikita katika Shughuli hizo lakini Bado hawajatambulika hivyo kuwepo kwa tuzo hizo zitasaidia kuwatambua wanawake wajasiriamali nchini na kuongeza wigo wa upatikanaji wa Mapato kwa Serikali.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza amesema kupitia tuzo hizo zitatambua na kuheshimu wanawake waliofanikiwa na wale wanaochipukia katika sekta za viwanda na biashara pia kujenga imani juu ya ujasiriamali na kuhamasisha wanawake na vizazi vijavyo kuwekeza na kujishughulisha katika shughuli za viwanda na biashara.

Post a Comment

0 Comments