Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Tanga Captain Christopher Shalua akizungumza na wavuvi na watumiaji wa vyombo vya usafiri baharini katika eneo la Kipumbwi wilayani Pangani wakati walipokwenda kutoa elimu ya usalama wanapotekeleza majukumu yao.
Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Tanga Captain Christopher Shalua akionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumika baharini kujiokolea wakati wavuvi na watumiaji wa vyombo vya usafiri baharini wanapokumbwa na majanga wanapotekeleza majukumu yao
Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Tanga Captain Christopher Shalua akisisitiza jambo kwa wavuvi na watumiaji wa vyombo vya usafiri baharini katika eneo la Kipumbwi wilayani Pangani wakati walipokwenda kutoa elimu ya usalama wanapotekeleza majukumu yao
Afisa Mkuu wa Vyombo Vidogo na Mabaharia kutoka Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) Captain Hamisi Mohamed Ally akzungumza jambo wakati wa utoaji elimu hiyo.
Sehemu ya wavuvi na watumiaji wa vyombo vya majini wakiangalia kifaa cha kujiokolea wakati wa utolewaji wa elimu hiyo
***********************
NA OSCAR ASSENGA, PANGANI.
SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewataka wenye vyombo vya kubebea mizigo baharini wakiwemo manahodha na mabaharia kuacha mara moja tabia ya kubeba abiria kwani kufanya hivyo wanavunja sheria na watakaobainika watakumbana na mkono wa sheria.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Tanga Captain Christopher Shalua wakati kikao chake na wanaotumia vyombo vya usafiri majini ikiwemo wavuvi kwenye maeneo ya Kipumbwi na Mkwaja.
Alisema eneo la kipumbwi limekuwa limekidhiri sana kwa vitendo ambavyo wenye vyombo na manahodha wamekuwa wakikiuka taratibu kutokana na kwamba vyombo vimepewa cheti cha kubeba mizigo lakini wanapakia na abiria.
Aidha alisema kufanya hivyo ni kosa kisheria na wakikamatwa watachukuliwa hatua kali iliwemo faini ya laki tano au kifungo cha miaka mitatu lakini pia kuhakikisha vinafikishwa mahakamani ili kuweza kushughulikiwa.
“Tukikamata chombo cha mizigo kinachobeba abiria tutakupiga faini au kukupeleeka mahakamani kwa vile vyombo sugu ambavyo vimekuwa na matukio ya kujirudia mara kwa mara lengo kubwa kuhaikisha vitendo vya namna hivyo vinakomeshwa lakini kwa kipindi cha mwaka jana watu nane wamefariki dunia kutokana na kupakia kwenye vyombo vinavyobeba mizigo”Alisema Captain Shalua.
Hata hivyo aliwataka watuamiaji wa vyombo vya usafiri majini wakiwemo manahodha na mabaharia ni vizuri wakachukua hatahadhari kwa kuhakikisha vyombo wanavyotumia vinakuwa na vifaa vya kujiokolea ili wanapokumbana na majanga mbalimbali baharini ikiwemo ya kuzama na mengine waweze kujiokoa.
Aidha alisema hivi sasa wanaendelea kutoa elimu kwa ajili ya wao kuchukua tahadhari ili wakikamatwa wasiseme hawajui hivyo watambue kwamba hawapaswi kupakia abiria kwenye vyombo vya mizigo.
“Tusije kuwakamataa halafu mseme kwamba mkibeba abiria kwenye vyombo vya kubebea mizigo ni makosa lakini pia haruhusiwi kubalisha jina mara baada ya kusajili awali bila mamlaka kujua”Alisema Captain Shalua.
Hata hivyo alisema suala lingine la muhimu kwenye vyombo vya usafiri majini ni lazima kuwepo na vifaa vya kujiokolea boya na vifaa vya kujiokolea na vile ambavyo vinatumia mafuta ni vizuri kuwa na vyombo vya kuzimia moto wanapokuwa majini vyombo.
Alisema kitu cha kwanza cha Msingi baada ya ujenzi wa vyombo vya usafiri majini ni kununua vifaa muhimu na unatakiwa kabla ya kufanya shughuli za majini kumuita Afisa Tasc ili kukiwezesha vyombo hivyo kukaguliwa na kuingia majini.
Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Afisa Mkuu wa Vyombo Vidogo na Mabaharia kutoka Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) Captain Hamisi Mohamed Ally alisema lengo la kikao hicho kilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya majini alisema lengo la kuja huko ni kuwapa elimu na kukumbushana suala la usalama kwenye vyombo vya majini ni kuwakumbusha usalama,
Alisema kwa sababu kikubwa ni kwamba kuna vyombo vimesajiliwa kwenye uvuvi kifanye jambo hilo na sio vyenginevyo na watakaobainika kufanya watashughulikiwa maana wapo watu ambao wamekuwa wakikiuka utaratibu ambao umewekwa na mamlaka husika .
Alisema kwa eneo la Kipumbwi wamekuwa wakisifika kwa kufanya mambo hayo kwa kuliangalia hilo serikali imekuwa na mwarobaini wake kwa kuwapelekea meli Tanga ili kuweza kuepusha hayo lakini baadhi yao wamekuwa bado wanaendelea na vitendo vya kupakia abiria kwenye vyombo vya mizigo hilo ni kosa kisheria.
“Lakini niwaambie kwamba chombo ambacho kimesajili kwa ajili ya kupakia mizigo mnapakia watu,hilo ni kosa kisheria hivyo ni muhimu kila chombo kifanye kazi yake kama ilivyokusudiwa kwa sababu mwaka jana ajali zilizotokea watu 8 walifariki ambao wanatokea maeneo ya Mkwaja na kipumbwi”Alisema Afisa huyo.
Hata hivyo alisema kuna vyombo vingi vya uvuvi vinafanya kazi zao lakini bado hawajakuja kujisajili kwenye mamlaka ya TASAC hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria kwani vinatakiwa kutambulika na mamlaka husika kabla ya kwenda kupata leseni ya uvuvi.
Afisa huyo alisema lengo la wao kutoa elimu hiyo ni kuwafahamisha ili waweze kutambua kwamba wanapaswa kuhakikisha vyombo ambavyo havijasajiliwa vinafanya hivyo ili wamiliki muweze kupata hati za kusaidia kuweza kupata mahitaji mengine muhimu.
Pia ili kuweza kuvijua vyimbo hivyo kwa urahisi kuweza kuwasaidia kwenye masuala ya usalama maana janga lolote linapotokea halimchagui mtu,tuwekeni utaribu mzuri vyombo vyao vinandikwe majini visizui na nambazi za usajili.
0 Comments