Taarifa za kusikitisha zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa Dkt. Mwele Ntuli Malecela amefariki dunia, leo Alhamisi, Februari 10, 2022, Geneva nchini Uswisi.
Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikuwa akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.
Kufuatia kifo cha Dkt. Mwele Ntuli Malecela, viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali wameshindwa kujizuia na kueleza masikitiko yao kufuatia msiba huo.
Balozi Hoyce Temu; Ofisi ya Uwakilishi @UbaloziGeneva imepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha Mtanzania mahiri na mchapakazi wa kitaifa na kimataifa #drmwele kilichotokea Leo hapa #Geneva #Uswisi. Pole sana kwa Familia na Watanzania wote hasa wanafamilia wa Geneva. #RIP
Mbunge Dk. Faustine Ndugulile; I am saddened by the death of Dr @mwelentuli earlier today. She was a sister, friend and confidant. Mwele was always on top of things. She played a critical role in my first Parliamentary campaign in 2010. I’ll remember her for her kindness. May her soul rest in eternal peace.
DC Jokate Mwegelo; Rest In Peace Dr. Mwele Red heartRed heartRed heart.
Maria Sarungi Tsehai; Broken heart I am absolutely floored! And still can’t believe it! Mwele! Loudly crying face. You accomplished many great things that some of us can only dream of. You worked hard and always followed the path of honesty. May God grant you a beautiful and peaceful eternal rest! Love and prayers to family.
Mbunge Ditopile; “Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dkt. Mwele Malecela aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI) pia alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) alikua Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele”
0 Comments