Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka hiyo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Emmanuel Manase akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari ,jijini Dar es Salaam.Mhariri wa Gazeti la Uhuru Jane Mihanji akichangia wakati wa Mkutano wa Wahariri na TCRA jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wahariri na watumishi wa TCRA katika mkutano wa kuangalia mafanikio ya utoaji huduma za Data wakati Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk.Jabiri Bakari akijibu hoja mbalimbali.
UPATIKANAJI wa gharama nafuu za data kwenye simu ni miongoni mwa mafanikio ambayo tafiti mbalimbali zimebainisha Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye gharama nafuu ya data. Uwekezaji kwenye Miundombinu na Sera nzuri ya Serikali kwenye Sekta ya Mawasiliano zimezesha upatikanaji wa huduma bora zenye gharama nafuu kwa wananchi.
Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali Jijini Dar Es Salaam, tarehe 22/02/2022, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri K. Bakari amewambia wahariri kwamba TCRA imekuwa ikitekeleza jukumu la kuweka mazingira rafiki katika ushindani wa utoaji huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha watoa huduma wanajenga ushindani wenye afya ili kuboresha utoaji huduma bora na nafuu kwa wananchi.
Dr. Jabiri amesema, Serikali kupitia TCRA, imewekeza na kujenga miundombinu yenyegharama kubwa iliyosaidia upatikanaji wa huduma za mawasiliano zilizobora kwa gharama nafuu Nchini ukilinganisha na nchi nyingine Barani Afrika na Ulimwenguni, tafiti mbalimbali zimebainisha.
Mathalani bei ya data kwa wastani wa 1GB ni Dola za Kimarekani (USD) 0.750 sawa na shilingi za Kitanzania TZS 1,725. Kielelezo 1 kinaonesha mlinganisho wa bei za data mwaka 2021. Tanzania ni nchi ya 6 miongoni mwa nchi 52, ambazo kiwango cha bei ya data kipo chini.
Kama ilivyo elezwa awali, Barani Afrika Tanzania imo miongoni mwa nchi Kumi kinara kwa unafuu wa gharama ya data inayotumika kwenye simu; hatua hii ni muhimu ikizingatiwa Serikali imekuwa ikiweka mazingira wezeshi ya uwepo watoa huduma wengi wa mawasiliano ya simu ili kushajihisha ushindani wenye manufaa kwa wawekezaji na kuwapatia wananchi unafuu wa gharama za mawasiliano unaotokana na mazingira ya ushindani kibiashara.
Tanzania inashika nafasi ya Sita kwa unafuu zaidi wa gharama ya data kati ya nchi 52 barani Afrika kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya utafiti iitwayo British Technology Research Firm.
Tanzania ni ya 6 kwa unafuu wa data miongoni mwa nchi 52 Baraki Afrika.
Pia Kielelezo 2, Kinaonesha mlinganisho Tanzania kuwa moja ya Nchi zenye bei nafuu ya data Duniani,
Kielelezo cha nafasi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye gharama nafuu ya data kwenye simu kwa kipimo cha gharama ya kila GB1. Tanzania ni ya 21 kati ya Nchi 155 duniani Chanzo: Cable.co.uk – worldwide mobile data pricing report 2021
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA amewahimiza wadau mbalimbali na watumiaji wa huduma na bidhaa za Mawasiliano kutumia fursa za kiuchumi zilizomo kwenye Sekta ya Mawasiliano kujiongezea kipato na kuboresha maisha. Dr Jabiri amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi na salama ya huduma za Mawasiliano, katika kujenga mshikamano miongoni mwa wananchi na kuleta Maendeleo ya Taifa.
0 Comments