Ticker

6/recent/ticker-posts

TAFITI ZA MAFUTA NA GESI ASILIA KUENDELEA MKOANI SINGIDA


********************

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amewapongeza wawakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) kwa mkakati wao wa kutoa elimu kwa viongozi na wananchi wa Mkoa huo hasa katika maeneo ambayo utafiti wa mafuta unafanyika.

Akitoa pongezi hizo leo 16 Februari 2022 ofisini kwake Dkt. Mahenge amesema endapo tafiti ambazo wanaendelea nazo zitakuwa na matokeo chanya zitasaidia kuongeza pato la taifa kupitia uuzaji wa mafuta na gesi ambayo yameonekana katika baadhi ya maeneo ya Singida na baadhi ya mikoa ya jirani.

Aidha amewahakikishia wataalamu hao kwamba Serikali ya mkoa itatoa ushirikiano wote utakaohitajika katika kufanikisha utafiti huo kwa kuwa miradi hiyo ikikamilika itakuwa na manufaa makubwa kwa wanachi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Awali akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa Mtaalamu wa utafiti wa mafuta na gesi Habibu Mohamedi kutoka Shirika hilo amesema Shirika linafanya utafiti katika kitalu cha Eyasi Wembere kilichopo Kaskazini.

Post a Comment

0 Comments