RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza akielekea Mkoani Mara kuhudhuria maziko ya mlinzi wake Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro aliyefar wiki hii.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimfariji na kumpa mkono wa pole Mama Mzazi wa Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro.Bi. Grace Mukakaro, baada ya kuwasili katika Kijiji cha Nyasusura Mkoani Mara kuhudhuria maziko hayo yaliofanyika leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwafariji Watoto na familia ya Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro, baada ya kuwasili Kijijini kwao Nyasusura Mkoani Mara, kuhudhuria maziko hayo yaliofanyika leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa salamu za pole kwa Wanafamilia na Ndugu wa Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro aliyekuwa mlinzi wake, wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu) MJANE wa Marehemu Kagere Bi. Gladeness Tandila akitowa heshima ya mwisho kwa marehemu mume wake Kagere wakati wa maziko yaliofanyika kijijini kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022, akisaidiwa na ndugu na jamaa.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro, aliyekuwa mlinzi wake, baada ya kuwekwa mwili wa marehemu wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu) WATOTO wa Marehemu Kagere wakiweka mchanga katika kaburi la baba yao wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa mlinzi wake marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro, yaliofanyika Kijijini kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu)
0 Comments