Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akifungua mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Zimamoto leo Jijini Dodoma.
Kamishna wa Polisi Uchunguzi wa Kisayansi (CP FB) Shabani Hiki, akizungumza wakati wa mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Zimamoto leo Jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa na wataalamu mnbalimbali katika Ukumbi wa Zimamoto leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washirikii mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akiteta jambo na Kamishna wa Polisi Uchunguzi wa Kisayansi (CP FB) Shabani Hiki wakati wa mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Zimamoto leo Jijini Dodoma.
**********************
Na Zena Mohamed,Dodoma.
NAIBU Waziri wa Wizara ya Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi Andrew Kundo amesema ili Jeshi la polisi likomeshe uhalifu wa kimtandao linatakiwa kuwekeza katika Teknolojia.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Andrew Kindo wakati akifungua mafunzo ya Makosa ya mtandao (CYBERCRIME)kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka(CRO) ammbapo amesema
Mafunzo hayo ni ya muhimu kwa Dunia ya leo ambayo imejawa na uhalifu kwasababu ya ongezeko la wabuni mbinu za uhalifu ni wengi na kila siku wanabuni mbinu mpya za uhalifu.
Amesema Kamati pamoja na mambo mengine ilipendekeza kutoa mafunzo hayo na serikali iliridhia mafunzo hayo ili kumfanya askari kuwa bora kwasababu mhalifu anaweza kuwa bora lakini askari anatakiwa awe bora zaidi.
"Lengo la jeshi letu kuwa la kisasa na linalojibu kiu ya watu katika utekelezaji wa huduma bora hivyo wananchi wanataikwa watambue nini maana ya makosa ya mtandao kupitia sisi kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini,"amesema.
Amesema Mafunzo hayo yanafanyika Morogoro,Dar es Salaam na Dodoma ili kulijengea uwezo jeshi la polisi nchini kuwa imara katika kutatua uhalifu wa kimtandao kupitia Teknolojia.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DCI),kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi(SACP)Deusdedit Nsimeki,alisema mafunzo hayo kupata uelewa mpana wa sheria ya makosa ya mtandao na kufanya taaluma hiyo katika kumsaidia mwananchi sio kujipatia kipato.
Amesema kumekuwa na malalamiko toka kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na kesi ya kupotelewa na simu zao kulipia gharama kubwa tofauti na simu ambayo imepotea na hivyo kuharibu taswira ya jeshi na taaluma kwa ujumla.
"Mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija na uadilifu katika utendaji kazi wenu ikiwa ninpamoja na kupambana na uhalifu na kupelekea kufanyakazi kwa ushirikiano mkubwa,"amesema.
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi uchunguzi wa kisayansi (CP)Shabani Hiki,alisema wao kama MA CRO ni kama msingi katika nyumba kwani taswira ya jeshi la polisi ipo kwao hivyo jukumu lao ni kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwa kupunguza malalamiko.
Amesema Kama watafanya kazi vizuri watasaidia kuondoa malalamiko toka kwa wananchi wale ambao huenda kwajili yakupata huduma katika masuala ya mashtaka.
0 Comments