MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akizungumza Bungeni Jijini Dodoma February 11,2022.MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akisisitiza jambo Bungeni Jijini Dodoma February 11,2022
******************************
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira ameiomba Serikali ipitie upya uamuzi wake wa kuiondoa masuala ya usalama wa chakula kutoka Wizara ya Afya na kuipelekea kwenye eneo la mambo ya viwanda na biashara badala yake wairudishe ilipokuwa awali .
Aliyasema hayo Bungeni Ijumaa tarehe 11 Februari 2022 Jijini Dodoma ambapo alisema kwa sababu duniani kote masuala ya usalama wa chakula yanaratibiwa na chini ya wizara ya afya kwa maana chini ya mamlaka ya kudhibiti ubora wa chakula na dawa na hata kwa Tanzania miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya hivyo chini ya TFDA.
Alisema hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali kufanya mapitio na maboresho ya uamuzi wake kwa kadiri itakavyoona hivyo kwa unyenyevu mkubwa na kwa maslahi mapana ya kulinda afya za Watanzania ,kulindi mzigo mkubwa ambao wizara ya afya unaona na mzigo wa ongezeko la magonjwa ya kansa ambao hauweleki suala la usalama wa chakula lirudi Wizara ya Afya.
Mbunge Neema alisema hata nchi za Afrika Mashariki zilikuja nchini kuja kujifunza lakini miaka ya karibuni serikali ilivunja mamlaka hiyo na badala yake kuunda TMDA na jukumu la usalama wa chakula wakaliweka chini ya Shirika la viwango (TBS) sasa jambo hilo limeweka maisha na afya za watanzania herani.
Alisema anasema hivyo kwa sababu TBS ina jukumu la kuangalia ubora wa matairi,misumari,mabati na nk na hapo hapo ipewe jukumu la kuratibu na kudhibiti ubora na usalama wa chakula na hao hao ndio wanatoa kibali kwa wazalishaji wa chakula .
“Na hao hao waende kuangalia kile kibali kimekidhi kutakuwa na mgongano wa maslahi, Mh Naibu Spika kuna jambo mahususi lilijitokeza ambalo ni dhihiri kwamba TBS haiwezi kuendelea kubeba jukumu la usalama wa chakula “Alisema
“Kwa mfano mwaka jana Octoba 2021 Shirika la chakula na madawa la Kenya lilitangaza kwamba linarudisha juice aina ya Ceres za Apple ambazo zilikuwa na aina moja ya sumu kuvu ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu mpaka siku hiyo kwa Tanzania TBS bado ilikuwa haijasema chochote”Alisema
Mbunge huyo alisema na gazeti la Mwananchi lilimtafuta Mkurugenzi wa TBS na anakumbuka alisema mpaka muda wa Octoba 16 mwaka 2021wamejiridhisha juice hizo zilikiwa hazijaingia nchini na wanaendelea kufuatilia na wakibaini zimeingia nchini zitazuiliwa .
Alisema hapo wakauambia umma kila kitu kipo sawa kwa masikitiko makubwa TBS waliwadanganya watanzania kwa sababu tarehe 22 kwenye kioski kimoja Jijini Dodoma alikuta juice hizo aina ya Ceres ya Apple yenye Barcode zile zile zinauzwa na alichukua jukumu la kuipiga picha na kumtumia waziri mwenye dhamana ya viwanga na biashara na uwekezaji ambaye alipokea na kusema atalifanyia kazi.
Aliongeza kwamba baada ya Waziri huyo kupokea alisema ataifanyia kazi hilo linaonyesha TBS hawakuchukulia kwa umakini jambo la usalama wa chakula na hawana muda wa kuangalia usalama wa chakula na wanahatarisha maisha ya watanzania kwa kuendela kulimbikiza mambo mengi ambayo mengine hayaendani na usalama wa chakula.
Kwa kuhitimisha Mbunge Neema Lugangira alisema kuwa jambo hili ni mahususi ambalo limejitokeza na linadhihiridha kwamba TBS haiwezi tena kuendelea kubeba usalama wa chakula wa watanzania.
Alisema kwa sababu mwezi Octoba 14 mwaka jana shirika la Chakula na Madawa la Kenya lilitangaza kwamba linarudisha juice ya Ceres ya Apple ambazo zilikuwa na aina moja ya sumu kuvu ambayo ilikuwa na hatari kwa maisha binadamu”Alisema
“Lakini mpaka siku hiyo TBS ilikuwa haijasema kitu chochote gazeti Mwananchi lilimtafuta Mkurugenzi wa TBS na nakumbuka alisema mpaka muda wa Octoba 16 mwaka 2021wamejiridhisha juice hizo zilikiwa hazijaingia nchini na wanaendelea kufuatilia na wakibaini zimeingia nchini zitazuiliwa”Alisema Mbunge Neema Lugangira.
Alisema hapo wakauambia umma kila kitu kipo sawa kwa masikitiko makubwa Naibu Spika TBS waliwadanganya watanzania kwa sababu tarehe 22 kwenye kioski kimoja Jijini Dodoma alikuta juice hizo aina ya Ceres ya Apple yenye Barcode zilikuwa zinauzwa na alichukua jukumu la kuipiga picha na kumtumia waziri mwenye dhamana ya viwanga na biashara na uwekezaji.
Hata hivyo alisema baada ya Waziri kulipokea alisema kwamba atalifanyia kazi na kwamba TBS hawachukulia kwa umakini usalama wa masuala ya chakula na hawana muda wa kuangalia masuala ya usalama na wanaendelea kuhatarisha maisha ya watanzania kwa kuendelea kulimbikiza mambo mengi ambayo hayaendani na usalama wa chakula.
"Kwa unyenyevu Mhe Naibu Spika naiomba Serikali ipitie upya uamuzi wake kuyaondoa masuala ya Usalama wa Chakula kwa maana ya Food Safety kutoka Shirika la Viwango TBS ambalo lipo chini ya Wizara inayosimamia masuala ya Viwanda na Biashara n.k. yaani turudi katika Best Practice na jambo hili lirudishwe Wizara ya Afya ili kuokoa na kulinda afya na maisha ya Watanzania, ”Alisema
0 Comments