Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiongoza viongozi mbalimbali, wananchi na wanafunzi katika zoezi la kupanda miti eneo la barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver Dodoma ikiwa ni utangulizi katika kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akipanda mti katika eneo la barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver Dodoma ikiwa ni utangulizi katika kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akipanda mti katika eneo la barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver Dodoma ikiwa ni utangulizi katika kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia zoezi la upandaji miti likifanywa na wanafunzi wa St. Peter Claver ikiwa ni utangulizi katika kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021. Februari 12,2022 leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki mara baada ya kumaliza kupanda miti katika eneo la barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver mkoani Dodoma ikiwa ni utangulizi katika kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021. Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akizungumza mara baada ya kumaliza kupanda miti katika eneo la barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver mkoani Dodoma ikiwa ni utangulizi katika kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021. Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,iliyozinduliwa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akielezea mikakati ya sera hiyo wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,iliyozinduliwa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ,akitoa salamu za mkoa huo wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,iliyozinduluwa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akitoa taarifa ya uzinduzi wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,iliyozinduluwa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Wilaya,Viongozi pamoja na wananchi wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,iliyozinduliwa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,uliozinduliwa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akionyesha mpango kazi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,mara baada kuuzindua leo Februari 12,2022 jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,Muongozo wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,mara baada ya kuizindua leo Februari 12,2022 jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Christina Mndeme,Muongozo wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,mara baada ya kuizindua leo Februari 12,2022 jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Athony Mtaka ,Muongozo wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,mara baada ya kuizindua leo Februari 12,2022 jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimkabidhi Mwandishi wa Fullshangwe blog,Alex Sonna,Muongozo wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 kwa niaba ya waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Christina Mndeme (kulia).Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 leo Februari 12,2022 jijini Dodoma.
................................................................
Na.Alex Sonna,DODOMA
MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa siku 30 kwa Waziri wa Nchi,Muungano na Mazingira,Selemani Jafo na Waziri wa TAMISEMI kuandaa mpango mkakati wa kukijanisha na kusafisha Mji wa Dodoma.
Maagizo hayo ameyatoa leo Februari 12,2022 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 ambapo Makamu huyo wa Rais amelitaka Jiji la Dodoma kuandaa mpango huo lengo likiwa ni kuifanya Dodoma iwe ya kijani.
“Ninataka taarifa ya utekelezaji ya huo wa mpango mkakati kiuhalisia niupate kila baada ya miezi mitatu sasa kwenye hili pale utekelezaji utakapotokea unalega lega natoa tahadhari wahusika wote wawajibike wenyewe kabla sijaingilia kati natumaini wamenisikia.
“Mfanye hivyo zoezi liwe endelevu na nataka niupate mpango huu ndani ya miezi mitatu tunataka Dodoma iwe kama Singapore lazima Dodoma iwe ya kijani lazima Dodoma iwe safi,”amesema.
Dk.Mpangpa amesema kuwa katika ziara zake zote atakazofanya , ajenda yake ya kwanza katika Mkoa husika itakuwa ni ujanishaji, upendezeshaji na usafi wa mazingira wa mahali hapo! Hata hivyo ameitaka NEMC, kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi vyanzo vya maji hususan katika mito na maeneo oevu nchini yasiendelee kuharibiwa.
''Kwa mfano, kwenye chanzo cha mto Ruaha katika Bonde la Ihefu, Mbeya, hakikisheni kuna matumizi endelevu ya mto huo pamoja na mito mingine nchini.''amesema Dk.Mpango.
Aidha amewataka Mawaziri wa Waziri wa Ardhi, Waziri wa Maji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kwenda kufanya tathmini na kumpa majibu hatua walizochukua katika ujenzi wa bwawa la mwalimu Nyerere.
''Siko tayari kama Makamu wa Rais kuona tunakamilisha ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere halafu baadae maji hayapatikani kutokana na uharibifu unaofanyika katika vyanzo vya mto Rufiji, tunafahamu kuwa shughuli za kilimo na mifugo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wetu lakini zifanywe bila kuvunja sheria za uhifadhi wa mazingira.''amesisitiza.
Kwa upande wake,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,Selemani Jafo amesema awali kulikuwa na sera ya mwaka 1997 ambayo ilipata mafanikio makubwa na kuzalisha sheria namba 20 ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Amesema kwa kuwa Sasa kwa sasa kuna mahitaji makubwa na matakwa mbalimbali ilisababisha waunde sera mpya ya mazingiraa ambayo imezinduliwa leo.
Amesema Juni 5 mwaka 2021,wakati Makamu wa Rais akizindua kampeni kapambe ya mazingira alitoa maelekezo ambayo ni pamoja na kuhakikisha sera ya mazingira inakamilika. Amesema kwa kupitia sera hiyo Tanzania inaenda kuwa sehemu salama katika suala la mazingira na kuungana na mataifa mengine.
“Sera hii itaenda kuongeza fursa za jinsi gani urejeshaji wa taka unaweza kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja ama vikundi mbalimbali hili ni jambo ambalo lipo katika sera yetu jinsi gani tutatumia mbinu mbadala taka zinarejeshwa,”amesema.
Amesema sera hiyo itaenda kuakisi hasa mabadiliko ya tabia nchi ambapo amemhakikishia Makamu wa Rais kwamba imezingatia Mpango wa Taifa wa miaka mitano 2020-21mpaka 2025-2026 mpango endelevu wa mwaka 2030 na mpango ule wa miaka 15 ulioanza mwaka 2011-2012 mpaka 2025-2026.
“Imani yetu mchakato wa sera hii utaenda kutekeleza masuala mbalimbali ambayo yataliokoa taifa letu hili na maelekezo yako ambayo umeyatoa muda wote kuhakikisha mazingira tunayatunza na tunayalinda kwa nguvu zote,”amesema.
Awali Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, amesema kuwa maandalizi ya sera mpya ya mwaka 2021 yametokana na changamoto za uharibifu wa mazingira zilizosababishwa na mabadiliko ya kiuchumi zilizosabishwa na taka zinazozalishwa mijini na taka zitokanazo na vifaa vya umeme na viumbe vamizi.
“Mchakato wa maandalizi wa sera ulihusisha wadau mbalimbali napenda kuwashukuru ninawaomba muendelee na ushirikiano huu,”amesema.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amesema wamekubaliana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) kupanda miti pembezoni mwa barabara ikiwemo katika ujenzi wa barabara za mzunguko wa nje katika Jiji la Dodoma.
0 Comments