Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AFUNGUA KONGAMANO LA 16 LA BONDE LA MTO NILE 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philipo Mpango akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam. Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Aweso akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam. Mchekeshaji ambaye huigiza sauti za viongozi Bw.Oscar akitoa burudani katika ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 kwenye viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam. Manaibu Waziri wakifuatilia ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam.kuanzia kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Hamad Hassan Chande, Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja na Naibu Waziri wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza. Wadau mbalimbali wa Bonde la Mto Nile wakifuatilia ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philipo Mpango akipata picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wa hapa nchini pamoja na wa nchi zinazopakana na Bonde la Mto Nile katika ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philipo Mpango akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Nile katika ufunguzi wa kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Idadi ya watu wanaoishi katika Bonde la Mto Nile imeendelea kuongezeka kutoka milioni 238 mwaka 2018 hadi milioni 278 mwaka 2022 hii ni takribani asilimia 10 ya watu wote Barani Afrika na zaidi ya watu milioni 300 hutegemea maji ya Mto Nile kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Ameyasema hayo leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philipo Mpango wakati akifungua kongamano la 16 la Bonde la Mto Nile 2022 katika viwanja vya Mlimani City Jijini dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Makamu wa Rais amesema ongezeko la idadi ya watu katika bonde la mto Nile lina maana kuwa, mahitaji ya maji pia yanaongezeka na uchafuzi wa maji katika bonde hilo yanazidi kuwepo.

"Hali hii inaweza kuamsha taharuki katika nchi zetu kwa kuogopa kuwa na upungufu wa maji na hivyo kusababisha nchi moja kufanya maamuzi yasiyo shirikishi ili kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya wananchi wake". Amesema Dkt.Mpango.

Aidha ameziomba na kuzisihi nchi wanachama kujadiliana pamoja matumizi bora na endelevu ya maji ya Mto Nile kwa faida ya nchi zote hali itakayosaidia kufikia muafaka wa pamoja ambao utakuwa endelevu na wenye manufaa kwa wote.

Amesema nchi Wanachama wanajukumu la kuhakikisha wanafikia malengo ya ushirikiano waliyojiwekea kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia rasilimali za maji ya Mto Nile, kwa kukumbuka kuwa miaka 20 iliyopita nchi wanachama walianza safari ya kuanzisha Kamisheni ya Bonde la Mto Nile kupitia Mkataba wa Ushirikiano wa Bonde la Mto Nile uliosainiwa na kuridhiwa na baadhi ya wanachama.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Aweso amesema Serikali ya Tanzania ipo bega kwa bega na nchi wanachama wa Umoja wa Bonde la Mto Nile katika kushirikiana masuala mbalimbali ya maendeleo ya umoja huo. Hata hivyo, Mhe. Aweso ameshauri umoja huo kuongeza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano katika shughuli za umoja huo sanjari na lugha za Kifaransa na Kiingereza.

“Asilimia 10% ya Waafrika wanategemea Bonde la Mto Nile, naamini kuimarika umoja wetu, tutaimarisha bara zima la Afrika na hata dunia kwa ujumla. Njia pekee ya kuimarika umoja huu, ni umoja na mshikamano wetu”, amesema Mhe. Aweso.

Post a Comment

0 Comments