Ticker

6/recent/ticker-posts

LHRC YAHIMIZA SERIKALI KUDHIBITI UFUNGIAJI HOLELA WA VYOMBO VYA HABARI



**************

Kituo Cha Sheria na haki za binadamu LHRC imekitaka kikosi kazi kitakachoundwa na waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari kupitia upya na kutekeleza maamuzi ya mahakama ya jumuiya ya afrika mashariki kuhusu Sheria ya huduma vyombo vya habari ya mwaka 2016 na kuhakikisha mchakato wa Sheria hizo unashirikisha wadau wote wa sekta hiyo.


Hatua hiyo inakuja mara baada ya waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Mh.Nape nauye hapo Jana Tarehe 10/02/2022 kufungulia magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa ambayo ni Tanzania Daima,Mwanahalisi,mawio na Mseto.

Akizungumza na waandishi mkurugenzi mtendaji wa LHRC Anna henga amesema hatua hiyo ni kiashiria kizuri Cha kurudi kwa huru wa vyombo vya habari,na ni Muda muafaka Sasa kuangalia changamoto za kiujumla za Sheria zinazokabili sekta ya habari na uhuru wa kujieleza.

"Ni ukweli kwamba Sheria hizi Bado zipo na zinaendelea kuumiza haki ya kupata taarifa kama ilivyoanishwa katika ibara ya 18 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1977,ambapo athari yake imeathiri magazeti,radio,televisheni,mitandao ya kijamii na uhuru wa internet" Alisema Bi Henga.

Aidha amesema kuwa LHRC ikiwa mdau mkubwa wa Sheria za habari,imefanya uchechemuzi kwa Muda mrefu tangu kuibuka kwa wimbi la utungaji wa Sheria zinazoweka ugumu kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake,pia kwa kiwango kikubwa Sheria hizo zimekwamisha urahisi wa upatikanaji wa taarifa kwa jamii.

"Miongoni mwa Sheria hizo ni Sheria ya makosa ya mtandao,2015; Sheria ya upatikanaji wa habari,2016;Sheria ya mamlaka ya mawasiliano pamoja na kanuni zake,na Sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016" Alisema Anna.

Kadhalika LHRC imewataka wadau wa habari kutoa maoni ya kina yatakayochangia kuboreshwa kwa Sheria za habari nchini.

Post a Comment

0 Comments